Wifi yangu na mama mkwe wake, all the way from Germany
Mimi na wifi yangu,sijui nini kilimfurahisha
The new me
Featured Posts
Thursday, 11 September 2014
Tuesday, 11 March 2014
Kipindi cha FAMILIA. Siku ya wanawake duniani
Photo Credits: happyholidays2014.com |
Kipindi hiki kilirushwa moja kwa moja (live) Jumamosi Machi 8, 2014
Katika kipindi cha wiki hii, mjadala ulijikita zaidi katika SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ambapo wageni Mary Ndaro akiwa Wichita Kansas na Mch. Tumaini Mwanyonga walijadili kwa mapana suala hili.
Wamegusa mengi mema ambayo ni muhimu kuyasikiliza.
Friday, 28 February 2014
TASWIRA KUTOKA SOKO KUU LA SANYA JUU MKOANI KILIMANJARO
Hii ni njia ya kuelekea soko hili ikiwa imejaa matope kutokana na kuwa katika kiwango cha changarawe |
Baadhi ya wachuuzi wakiwa sokoni hapo kununua mahitaji yao lakini mazingira ya soko hayaridhishi kutokana na uchafu uliokithiri hapo na kuhatatrisha afya za walaji wa bidhaa |
hali halisi inavyonekana sokoni hapo baada ya mvua kunyesha |
Msimu huu wa mvua unasababisha kero hii kwa baadhi ya wateja hata wafanyabiashara sokoni |
hali hii pia ni kero kwa watembea kwa miguuu sokoni hapo |
Picha zote na mdau Wito Msafiri wa Mwanaharakati Mzalendo Blog |
[AUDIO]: Kipindi cha familia kutoka Jamii Productuion...BAJETI KATIKA FAMILIA (Pt II)
Photo credits: moneymanagement.org
Karibu katika kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production.
Katika kipindi hiki, tumeingia katika sehemu ya pili ya mjadala kuhusu BAJETI KATIKA FAMILIA ambapo mbali na historia ya bajeti, pia tumesisitizwa kuhusu umuhimu wake, namna ya kulitekeleza na mengine mengi.
Wachangiaji studio walikuwa ni Amos Cherehani ambaye ni mtaalamu wa masuala ya fedha, Denzel Musumba na Mubelwa Bandio
KARIBU UUNGANE NASI

Wednesday, 26 February 2014
[AUDIO]: DAKIKA 90 ZA DUNIA: Kwanini Facebook imetumia dola bilioni 19 kununua WhatsApp?
Photo: Mobile88.com
Kama wewe ni mmoja wa wanaotumia njia ya mawasiliano iliyojipatia umaarufu ya WhatsApp, basi ujue kuwa nawe ni miongoni mwa wateja takribani nusu bilioni walioufanya mtandao huo kuwa maarufu zaidi duniani kwa kipindi kifupi tu.
Ni umaarufu huu uliofanya kampuni kubwa ya mawasiliano ya Facebook wiki hii kuona umuhimu wa kutumia dola za kimarekani bilioni 19 kununua WhatsApp.
Lakini kwanini kampuni itumie kiasi hicho kikubwa kwa kampuni kama hii?
Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).Kama wewe ni mmoja wa wanaotumia njia ya mawasiliano iliyojipatia umaarufu ya WhatsApp, basi ujue kuwa nawe ni miongoni mwa wateja takribani nusu bilioni walioufanya mtandao huo kuwa maarufu zaidi duniani kwa kipindi kifupi tu.
Ni umaarufu huu uliofanya kampuni kubwa ya mawasiliano ya Facebook wiki hii kuona umuhimu wa kutumia dola za kimarekani bilioni 19 kununua WhatsApp.
Lakini kwanini kampuni itumie kiasi hicho kikubwa kwa kampuni kama hii?
Hii ilikuwa ripoti ya Februari 22, 2014
MAKAMU WA CCM BARA MH.PHILIP MANGULA AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO BEIJING CHINA
MH.Mangula akibadilishana mawazo wadau Joel Kayombo na Shauku Kihombo ambao wapo nchini humo kwa masomo katika moja ya vyuo vinavyopatikana mjini Beijing China |
Monday, 10 February 2014
Kipindi cha familia kutoka Jamii Productuion...BAJETI KATIKA FAMILIA
Bwn Solomon, Sunday Shomari na Herriet Shangirai wakijadili jambo ndani ya studio za Jamii Production. Washington DC
Karibu katika kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production.
Katika kipindi hiki, tumejadili suala la BAJETI KATIKA FAMILIA.
umuhimu wake, namna ya kulitekeleza na mengine mengi.
Wachangiaji studio walikuwa ni Herriet Shangirai, Sunday Shomari, Solomon na Mubelwa Bandio

Rekodi katika michuano ya Olimpiki Sochi
Michuano ya 22 ya Olimpiki ya majira ya baridi imeanza jana huko Sochi nchini Russia.
Mabadiliko mengi yametokea katika miaka sita na nusu ya maandalizi yake
Na wakati mamilioni ya watu duniani wakiwa wameelekeza macho na masikio yako huko, kujua nani atashinda nini na nani atavunja rekodi gani, tayari rekodi kubwa zaidi katika michuano hiyo imevunjwa hata kabla ya kuanza kwake.
Na tuipitie safari safari ya maandalizi ya michuano hii mpaka ilipofikia na baadhi ya vikwazo ilivyopambana navyo
Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Saturday, 18 January 2014
Thursday, 2 January 2014
MAKAMU BALOZI WA ZAMBIA NA WAFANYAKAZI WA TIGO WASHEREKEA MWAKA MPYA NA WATOTO YATIMA
Baadhi ya wafanyakazi kampuni ya simu Tigo toka tawi la Mliman City wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima toka kituo cha Islamic orphans home care kilichopo Mbweni wilaya ya Bagamoyo ambapo walipata chakula cha mchana na kutoa baadhi ya misaada kwa ajili ya watoto hao wanaolelewa katika kituo hicho wakishiriiana na makamu balozi wa Zambia Bi Elizabeth Phill
baadhi ya watoto kutoka kituo hiki cha mwandaliwa wakiwa na sura za furaha baada ya kufarijiwa na ujio wa wafanyakazi wa tigo na makamu balozi wa zambia bi elizabeth phill
watoto yatima wakipata chakula pamoja na makamu balozi wa Zambia Bi Elizabeth Phill na wafanyakazi wa tigo toka tawi la Mliman city |
baadhi ya watoto kutoka kituo hiki cha mwandaliwa wakiwa na sura za furaha baada ya kufarijiwa na ujio wa wafanyakazi wa tigo na makamu balozi wa zambia bi elizabeth phill
Makamu balozi wa Zambia bi Elizabeth Phill akifurahia jambo na mmoja wa watoto toka kituo hicho cha Mwandaliwa Islamic orphans and homecare kilichopo MBWENI |
Mmiliki wa kituo cha watoto yatima cha Mwandaliwa islamic orphans and homecare bi halima ramadhani akiwa na mmoja wa watotoyatima wanaotunzwa na kituo hicho |
Mmiliki wa kituo hicho cha watoto yatima bi halima ramadhani akiwa katika picha ya pamoja na makamu balozi wa ZAMBIA NA wafanyakazi wa tigo toka tawi la MLIMANI CITY baada ya kusherekea mwaka mpyaa |
Makamu balozi wa Zambia bi elizabeth phill akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo hicho PICHA ZOTE NA MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG |
Subscribe to:
Posts (Atom)