Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Sunday, 1 November 2009

WALIMU KUGOMA TENA NCHI NZIMA

Chama cha walimu Tanzania (CWT)Kimetangaza mgomo wa walimu nchi nzima kuanzia novemba 7mwaka huu 2009,kutokana na kutolipwa kikamilifu madeni yao wanayoidai serikali.Walimu wanadai madeni mengi ikiwa ni pamoja na fedha za malimbikizo ya mishahara,uhamisho, likizo,malipo ya kwenda masomoni na mengineyo.

mgomo huo utahusisha walimu wote wa shule za msingi sekondari,vyuo vya ualimu na wakaguzi wa shule.pamoja na hayo walimu watatakiwa kwenda mashuleni kama kawaida ila hawataingia darasani, badala yake watakaa maofisini na kujadili hatima ya malipo yao.Huu utakuwa ni mgomo mwingine ukiacha ule wa novemba mwaka jana,uliozimwa na mahakama kuu divisheni ya kazi novemba 17,ambapo walimu walidai jumala ya bilioni 50.

Inashangaza kuona wabunge wakipokea posho mara mbili mbali na mishahara yao,huku serikali ikisahau madeni ya walimu hii inaonyesha serikali haiwajali waliamu kabisaaaaaa,
Alafu tunategemea walimu hao hao watoe wataalamu.

0 comments: