Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Featured Posts

Waving Tanzania flag

Thursday 11 September 2014

OOOOH! HOW I MISSED YOU GUYZ.

 Wifi yangu na mama mkwe wake, all the way from Germany
 Mimi na wifi yangu,sijui nini kilimfurahisha
 The new me

Tuesday 11 March 2014

Kipindi cha FAMILIA. Siku ya wanawake duniani

Photo Credits: happyholidays2014.com
Karibu katika kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production.
Kipindi hiki kilirushwa moja kwa moja (live) Jumamosi Machi 8, 2014
Katika kipindi cha wiki hii, mjadala ulijikita zaidi katika SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ambapo wageni Mary Ndaro akiwa Wichita Kansas na Mch. Tumaini Mwanyonga  walijadili kwa mapana suala hili.
Wamegusa mengi mema ambayo ni muhimu kuyasikiliza.

Friday 28 February 2014

TASWIRA KUTOKA SOKO KUU LA SANYA JUU MKOANI KILIMANJARO

Sanya Juu ni mji mdogo ndani ya wilaya Siha Mkoani Kilimanjaro ikiwa ni Km 25 toka Bomang'ombe  na KM 50 toka Moshi Mjini, weekend hii nilifanikiwa kuutembelea Mji wa Sanya Juu ambapo siku ya Jumamosi  mji huu huwa umechangamka kwa shamrashamra za kibiashara. katika pita pita zangu nilifanikiwa kulitembelea soko ila nilishangazwa na hali niliyo ikuta ya miundombinu isiyo kidhi na kulifanya soko kuonekana hatarishi kwawafanya biashara na wateja wao kiafya.
Huu ni msimu wa mvua kwa sehemu kubwa ya mkoa wa Kilimanjaro, hatua za haraka zinatakiwa kuchukuliwa kuimarisha miundombinu ya soko la Sanya Juu kuimarisha afya za wafanyabiashara na wateja wao. 

Hii ni njia ya kuelekea soko hili ikiwa imejaa matope kutokana na kuwa katika kiwango cha changarawe

Baadhi ya wachuuzi wakiwa sokoni hapo kununua mahitaji yao lakini mazingira ya soko hayaridhishi kutokana na uchafu uliokithiri hapo na kuhatatrisha afya za walaji wa bidhaa

hali halisi inavyonekana sokoni hapo baada ya mvua kunyesha

Msimu huu wa mvua unasababisha kero hii kwa baadhi ya wateja hata wafanyabiashara sokoni 

hali hii pia ni kero kwa watembea kwa miguuu  sokoni hapo 

Picha zote na mdau Wito Msafiri wa Mwanaharakati Mzalendo Blog

[AUDIO]: Kipindi cha familia kutoka Jamii Productuion...BAJETI KATIKA FAMILIA (Pt II)

Photo credits: moneymanagement.org
Karibu katika kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production.
Katika kipindi hiki, tumeingia katika sehemu ya pili ya mjadala kuhusu BAJETI KATIKA FAMILIA ambapo mbali na historia ya bajeti, pia tumesisitizwa kuhusu umuhimu wake, namna ya kulitekeleza na mengine mengi.
Wachangiaji studio walikuwa ni Amos Cherehani ambaye ni mtaalamu wa masuala ya fedha, Denzel Musumba na Mubelwa Bandio
KARIBU UUNGANE NASI

Wednesday 26 February 2014

[AUDIO]: DAKIKA 90 ZA DUNIA: Kwanini Facebook imetumia dola bilioni 19 kununua WhatsApp?

Photo: Mobile88.com
Kama wewe ni mmoja wa wanaotumia njia ya mawasiliano iliyojipatia umaarufu ya WhatsApp, basi ujue kuwa nawe ni miongoni mwa wateja takribani nusu bilioni walioufanya mtandao huo kuwa maarufu zaidi duniani kwa kipindi kifupi tu.
Ni umaarufu huu uliofanya kampuni kubwa ya mawasiliano ya Facebook wiki hii kuona umuhimu wa kutumia dola za kimarekani bilioni 19 kununua WhatsApp.
Lakini kwanini kampuni itumie kiasi hicho kikubwa kwa kampuni kama hii?
Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Hii ilikuwa ripoti ya Februari 22, 2014

MAKAMU WA CCM BARA MH.PHILIP MANGULA AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO BEIJING CHINA

Makamu wa ccm bara MH.Philip Mangula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watanzania wanaosoma na kufanya kazi nchini China katika mji wa Beijing baada ya kukutana nao kwa kikao kifupi katika kujadili mstakabali wa wasomi katika ujenzi wa taifa lao.Hii ilifanyika baada ya ziara fupi nchini aliyofanya MH,Mangula mwanzoni wa wiki hii.

Baadhi ya watanzania waishio nchini wakiwa katika picha ya pamoja na makamu wa ccm, bara MH.Philip Mangula
baada ya kikao cha kujadili mambo kadhaa ya mstakabali wa nchi yao katika ziara fupi aliyofanya mwanzoni wa wiki hii. 


MH.Mangula akibadilishana mawazo wadau Joel Kayombo na Shauku Kihombo ambao wapo nchini humo kwa masomo  katika moja ya vyuo vinavyopatikana mjini Beijing China 
                     PICHA ZOTE NA MDAU SHAUKU KIHOMBO 

Monday 10 February 2014

Kipindi cha familia kutoka Jamii Productuion...BAJETI KATIKA FAMILIA

Bwn Solomon, Sunday Shomari na Herriet Shangirai wakijadili jambo ndani ya studio za Jamii Production. Washington DC
Karibu katika kipindi cha FAMILIA kutoka Jamii Production.
Katika kipindi hiki, tumejadili suala la BAJETI KATIKA FAMILIA.
umuhimu wake, namna ya kulitekeleza na mengine mengi.
Wachangiaji studio walikuwa ni Herriet Shangirai, Sunday Shomari, Solomon na Mubelwa Bandio
KARIBU UUNGANE NASI

Rekodi katika michuano ya Olimpiki Sochi

Michuano ya 22 ya Olimpiki ya majira ya baridi imeanza jana huko Sochi nchini Russia. Mabadiliko mengi yametokea katika miaka sita na nusu ya maandalizi yake Na wakati mamilioni ya watu duniani wakiwa wameelekeza macho na masikio yako huko, kujua nani atashinda nini na nani atavunja rekodi gani, tayari rekodi kubwa zaidi katika michuano hiyo imevunjwa hata kabla ya kuanza kwake. Na tuipitie safari safari ya maandalizi ya michuano hii mpaka ilipofikia na baadhi ya vikwazo ilivyopambana navyo Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Thursday 2 January 2014

MAKAMU BALOZI WA ZAMBIA NA WAFANYAKAZI WA TIGO WASHEREKEA MWAKA MPYA NA WATOTO YATIMA

 Baadhi ya wafanyakazi kampuni ya simu Tigo  toka tawi la Mliman City wakiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima toka kituo cha Islamic orphans home care kilichopo Mbweni wilaya ya Bagamoyo ambapo walipata chakula cha mchana na kutoa baadhi ya misaada kwa ajili ya watoto hao wanaolelewa katika kituo hicho wakishiriiana na makamu balozi wa Zambia Bi Elizabeth Phill


watoto yatima wakipata chakula pamoja na makamu balozi wa Zambia Bi Elizabeth Phill na wafanyakazi wa tigo toka tawi la Mliman city








baadhi ya watoto kutoka kituo hiki cha mwandaliwa wakiwa na sura za furaha baada ya kufarijiwa na ujio wa wafanyakazi wa tigo na makamu balozi wa zambia bi elizabeth phill


Makamu balozi wa Zambia bi Elizabeth Phill  akifurahia jambo na mmoja wa watoto toka kituo hicho cha Mwandaliwa Islamic orphans and homecare kilichopo MBWENI






Mmiliki wa kituo cha watoto yatima cha Mwandaliwa islamic orphans and homecare bi halima ramadhani akiwa na mmoja wa watotoyatima wanaotunzwa na kituo hicho


Mmiliki wa kituo hicho cha watoto yatima bi halima ramadhani akiwa katika picha ya pamoja na makamu balozi wa ZAMBIA NA wafanyakazi wa tigo toka tawi la MLIMANI CITY baada ya kusherekea mwaka mpyaa


Makamu balozi wa Zambia bi elizabeth phill akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo hicho 
PICHA ZOTE NA MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG