Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, 15 December 2009

Wajumbe Copenhagen watofautiana.

Mgawanyiko umetokea kwenye kongamano la kimataifa la mabadiliko ya hali ya anga kati ya nchi masikini na nyingine zinazotoa viwango vya juu vya gesi inayochafua mazingira.
Bara Afrika na nchi nyingine zinazoendelea zimelalamikia kwamba mapendekezo yao yamepuuzwa.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya mazingira amesema kuna hofu dhidi ya nchi tajiri za bara Ulaya,Marekani, Uchina na India kwamba huenda zikashinikiza mkataba ambao hautazishuritisha kupunguza viwango vya gesi ianyochafua mazingira.

Nchi masikini zimependekeza viwango vya kupunguza gesi hiyo vizingatie muafaka wa Kyoto ambao umeweka masharti makali ya kupunguza gesi inayochafua mazingira kwa nchi tajiri.

Denmark ambayo ni mwenyeji wa kongamano hilo imepuuza lalama za nchi masikini akizitaja kama sarakasi.

Mwandishi wa BBC anasema hata hivyo viongozi wa dunia wanaowasili kwa kongamano hilo juma hili hawataki kukumbwa na aibu ya baadhi ya nchi kususia mkutano huo.
Source BBCswahili.com

0 comments: