Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Monday 25 January 2010

Wanaume Wa kichina Hatarini kukosa Wenza!!


Mwishoni mwa miaka ya 1970 China ilipitisha sheria ya kuzaa mtoto Mmoja katika kila familia, lengo lilikuwa ni kupunguza idadi ya watu nchini humo.Na familia nyingi walipendelea mtoto wa kiume wakiamini akikua atawasaidia wazazi wake tofauti na mtoto wa kike,wazazi walichofanya ikionekana mimba ni ya mtoto wa kike basi mimba hiyo ilitolewa haraka.Matokeo yake sheria hiyo imepelekea kuwa na wanaume wengi zaidi kuliko wanawake kwa sasa nchini China.Inasemekana katika miaka 10 ijayo wanaume millioni 24 wa Kichina huenda wakajikuta wanakosa wanawake wa kuwaoa...Hivi thamani ya mtoto wa kike itakuja onekana lini? katika mabara haya mawili Asia na Africa.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nchi bila wanawake!! Ni swali nzuri nanukuu "Hivi thamani ya mtoto wa kike itakuja onekana lini? katika mabara haya mawili Asia na Africa."

chib said...

Itaonekana iwapo wanawake nao watajithamini zaidi kuliko sasa.
Hivi hauoni ajabu maofisini kukiwa na rabsha btn akina dada, wao wenyewe utasikia ... unajua wanawake hatupendani....
Ni maoni na mtazamo tu,