Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday 23 March 2010

WHY MEN CHEAT?

Have you cheated? Have you forgiven a straying spouse? Janny McCarthy want to know why men cheat?........ hata mimi pia nataka kujua kwanini wanaume huongopa sana hususani katika mapenzi? Sio kwamba wanawake hawacheat nooo! do not get me wrong.....najua wanaume watanishambulia ila nataka tu kujua kwa wale wanaofahamu sababu au kwanini wanaume wanaongopa sana kwenye mapenzi?

6 comments:

chib said...

Just be aware.. that men who will attempt to give an answer to this question... certainly they will cheat you.
Enjoy your decision and curiosity!!

EDNA said...

Hahaaa Chib...hope not, but let`s wait n see.

Simon Kitururu said...

Kuna sababu nyingi na sirahisi kurahisisha jibu kwa kuwa kila afanyaye mchezo wakutoka nje ya mahusiano huwa na sababu zake binafsi.

Lakini kuna wadaio historia ya BINADAMU inaonyesha kuwa TABIA za BINADAMU ni matokeo ya maelfu ya miaka na vizazi vingi hasa kutokana na BINADAMU alivyokuwa anakabiliana na mazingira yake.

Kwa hiyo hata tabia ya binadamu ya kuogopa nyoka au buibui huwa imejengeka katika Binadamu hata ambaye hajui nyoka au buibui kutokana na jinsi alivyorithi tabia kwa vizazi vilivyopita.

Kwa hiyo kihistoria inaonyesha BINADAMU hakuwa na mwanamke au mwanaume mmoja. Na tabia ya kuona akuvutiaye na kujikataza kuonja ni tabia mpya kwa BINADAMU ndio maana hata katika stori hata za juzijuzi tu baada ya binadamu kuanza kuandika kama vile za BIBLIA utakuta wajanja wote watukufu hawakuwa na mwanamke mmoja na ilikuwa kawaida. Kwa kifupi kutotoka nje ni tabia mpya kwa binadamu na kwa maelfu ya miaka kutoka nje ya mahusiano ndio ilikuwa kawaida kwa binadamu

Kutokuwa na mtu mmoja inasemekana ilikuwa ni moja ya aina ya kukabili mazingira. Kwanza wanawake wengi walikufa baada ya kujifungua na kwa wanawake ilikuwa ni ujanja kubadilibadili wananaume ili kuhakikisha wanapewa mimba na vijeba wenye afya na wawezao kuwahudumia katika kipindi ambacho mafanikio ya binadamu yalipimwa kwa kuwa na watoto tu na kuweza kuwalisha NA KULENGA RIJALI MWENYE NGUVU tofauti ilichangia kuongezea uwezekano wa kupata mtoto mwenye afya ambaye atakabili mazingira na kuishi hasa ukizingatia hata wanaume wenyewe maisha yao yalikuwa sio marefu kihivyo kutokana na ugumu wa mazingira.

Ok kuna huo mtazamo hasa kutoka kwa baadhi ya wanahistoria walaliao katika kuangalia ni lini hasa imegeuzwa kuwa kila binadamu awe na limtu limoja tu wakati kwa siku anaweza kuvutiwa na watu mia ambao labda mazingira yangeruhusu mtu angeonja mwingine bila kuathiri mtu.

Pili kuna wadaio KIBAOLOJIA watu wametengenezwa ili watamani ku-cheat na ni tabia za KIJAMII tu ZAKUJIFUNZA ambazo dini na tamaduni hucheza katika hilo ambazo huzuia watu kufanya kweli kwa kuwaumiza Kisaikolojia.

Kibaolojia mwanamume na mwanamke wameumbwa watamaniane na ni kasoro kama unamuona mtu umpendaye afaaye kwa penzi kama mahormoni na ubongo visipokuwa vinasaidia moja ya wazo lako ni kufikiria anafanyaa kwa penzi. Na kikuzuiacho ku-cheat ni tabia za kujifunza .

Sasa swali:
Why do men cheat?

JIBU lenye swali:

Why do anybody think it is supposed to be normal if men don't cheat?

Na inawezekana ni ushindi tu wa Baoloji na Kemia ya BINADAMU ambayo huzalisha kupenda, kutaka na hata kusikia utamu kwa mtu ukilinganisha na MAADILI mapya watu waliyojifunza juzi juzi ndio yatakayosababisha mtu baada ya kufikisha wake wanne wa kihalali ndani ya dini tukufu ya kiislamu kushindwa kujikontrol kwa kuogopa dhambi kwa kuwa maadili ya kuogopa dhambi ni dhaifu na kuonja nje ya hao wanne WAKE WAZURI wa kihalali kwa amri ya mwili au kuusikiliza mwili badala ya kitabu kitakatifu na jamii inasema nini.

Unafikiri ni lini Binadamu hustukia ni maadili mazuri kuwa na mtu mmoja tu?

Samahani kwa mlolomo mrefu!:-(

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Pengine utafiti huu unatoa fununu kidogo kuhusu suala hili.

http://matondo.blogspot.com/2009/06/are-men-wired-to-cheat.html

Na mimi nasubiri...

Anonymous said...

hahahahahah, kwa sababu wanawake mko wengi, sasa hao wengine watapata wapi starehe ya maisha

Mdau

Mzee wa Changamoto said...

Sina performance nzuri kwenye hesabu lakini hizi za kudokoa naziweza kiasi.
Nililosikia ni kuwa mwanamme mmoja anaweza kuwa na mahusiano na wanawake 4. Kwa hiyo uwiano hapo ni 1/4.

Anyway, labda niache hesabu nirejee kwenye HULKA. Si unajua kuwa watu hutapanya pesa pale wanapokuwa nazo na palipo na uwezekano wa kupata kitawanyicho? Ina maana kinadada (ambao mara zote huonekana kukerwa na tabia hizi za wanaume) wakijifunza kusema NO, basi wanaume watakosa pa kwenda na kama WATALAZIMIKA KUNANILII NJE (Mungu aepushe) basi wakuwa na wanaume wenzao.
Lakini najua kama una hela na hakuna cha kununua, huwezi kununua kitu.
Nadhani URAHISI WA UPATIKANAJI WA KINADADA NA KUTOTAKA KUTAMBUA KUWA WAO NI SEHEMU YA TATIZO kunawafanya kupuuzia njia pekee inayoweza kusaidia kuzuia hili.
Ndio maana niliwaza kwanini watu walimkandamiza Tiger Woods kwa ku-cheat dhidi ya mkewe na kutohoji chochote kuhusu wale kinadada / kinamama zaidi ya 13 ambao walijua kuwa Tiger ameoa na wakaendelea kuwa na mahusiano naye?
Nawaza hili kama suala ambalo lahitaji kuangaliwa kwa JICHO LA NDANI na tukifanya hivyo tutagundua kuwa ama lawama ziko sawa ama wanawake wanahitaji lawama zaidi kwa "kujirahisisha"

Anyway
NAWAZA KWA SAUTI TU.