Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Friday, 21 May 2010

THANK GOD IT`S FRIDAYYYY!ALLERGY NI NINI?


Kwa wale wenye matatizo ya ALLERGY kama mimi huenda wakawa wanajiuliza allergy ni nini? na husababishwa na nini? na je kuna dawa yoyote ya kuzuia? je allergy ni ugonjwa kama magonjwa mengine? na kila binadamu ana allergy?.
Kuna wengine wakikaa sehemu za vumbi watapiga chafya mpaka utaona huruma,wengine manyoa ya paka yakigusana na ngozi basi si kuwashwa huko,wengine perfumes na vingine vingi.Binafsi nikila samaki fulani mwili wote hutoka mapele ya ajabu ajabu,cha ajabu mpaka leo sijawahi kujua ni aina gani ya samaki nina allergy naye,hivyo nakula kila aina ya samaki mpaka nimpate huyo adui yangu.Sababu iliyonifanya niulize maswali yote haya ni juzi tu mimi na rafiki yangu tulienda mtembelea rafiki yetu, bahati mbaya ile nyumba wanapaka kama watatu hivi,basi jamaa kuona tu wale paka akatoka mbio huku akijikuna kuuliza akasema anaallergy na paka na hawezi kuingia tena nyumba ile...alitia huruma kwa kweli...hii ikanifanya nikumbuke matatizo yangu na samaki miaka michache ya nyuma.
Kwa wale wenye ufahahamu zaidi kuhusu allergy tafadhali tusaidie kujibu maswali hayo.

1 comments:

Candy1 said...

that makes two of us coz sometimes napata reactions kama hivyo kupiga chafya, kuwashwa mwili mzima then nikijikuna mwili kama unatutumka hivi, sielewi, naendelea na research pia nijue nini hakinipendi