Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday, 14 October 2010

HAPPY BIRTHDAY STRIVE FOR LIFE.

Wakati Watanzania ulimwenguni kote tunakumbuka siku ambayo Baba wa Taifa Mwl Julias Kambarage Nyerere alitutoka…Mimi nasherehekea kuzaliwa kwa blog yangu ya STRIVE FOR LIFE.
Tarehe kama ya leo mwaka mmoja uliopita blog hii ilianzishwa rasmi.Siku zinakimbia jamani eti tayari ni mwaka mmoja mweee.
Nitakuwa ni mchoyo wa shukrani endapo sitawashukuru wasomaji wangu, maana nyinyi ndio mliofanikisha uwepo wa Blog hii.Waswahili wanasema shughuli ni watu na watu wenyewe ni nyinyi.
Shukrani za dhati zimuendee Adam wa blog ya MKONO WANGU BLOG yeye ndiye mtu wa kwanza kunikaribisha kupitia blog yake asante sana mkuu… MZEE WA CHANGAMOTO asante sana kaka
Kwani wewe ndiye uliyenifundisha jinsi ya kuweka Video hapa bloguni, baada ya kuhangaika kwa muda mrefu bila mafanikio, naheshimu na kuthamini mchango wako…DADA YASINTA wewe ndie mtu wa kwanza kucomment hapa …,nilifurahi sana siku uliyocomment i was like waooh kumbe kuna watu wanapita hapa?
SIMON KITURURU a.k.a Matakatifu hongera kwa kiswahili chako kilichowazi na staili ya uandishi wako, nikisomaga maneno yako mie hoi asante kwa kuonyesha upendo na ushirikiano kaka.
PROF MASANGU MATONDO heshima kwako na asante kwa kupita hapa mwabeja sana lol ..sijui nimepataia mwanawane?, CANDY 1 LITTLE WORLD, thanks lil sis for passing by.
KAKA CHIB wherever you are thanks for showing some love.
KAKA CHACHA WAMBURA comment zako zilizojaa utani huwa zinaniacha hoiiii asante sana pia kwa kupita hapa.
MIRAM3 hivi tule tustory unatutoaga wapi? maana tunavutia ile mbaya,asanate nawe kwa kukanyaga mahali hapa.
ADELA mdada.... asante na wewe kwa kupita mahali hapa.
PASSION4FASHIONTZ ,JOHN MWAIPOPO, EDWIN NDAKI, FADHY MTANGA, MUMYHERY,EVA JAMES, KAERO MKUNDIasanteni pia.
Natamani ningewaorodhesha wote hapa ila kwa kufanya hivyo itanichukua siku nzima.Samahani sana kwa wale ambao sikuwataja nawapenda wote..
THANK YOU ALL FOR MAKING IT HAPPEN.

5 comments:

SIMON KITURURU said...

Hongera sana Edna! Viva STRIVE FOR LIFE blog!

Yasinta Ngonyani said...

Ni furaha ilioje kupata heshima kama hii hapa kibarazani pa Strive for Life. Na pia napenda kusema HONGERA SANA kwa kutimiza LIMWAKA. na pia nakutakia kila jema na pia nina imani limwaka limepita na tutapata mambo mapya...lol

Candy1 said...

You are welcome big sis :-), you know how it works! But many congrats! It is not an easy job to survive 365 days with a blog that is alive, keep going dada!

Anonymous said...

hongera kwa kutimiza mwaka.

chib said...

Hongera sana kwa kutimiza mwaka mmoja wa ku-blogu, najua nimewahi kabisa, kwani huku kwangu tar 14 haijapita, Kama kawaida, huwa sikosi kupita hapa hata kama mtandao ninaotumia unachechemea