Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, 19 October 2010

KISWAHILI!

Bango likiwa na ujumbe unaosomeka "SISI SOTE TUPIGANISHE UBAKAJI" Sina hakika kama neno TUPIGANISHE ni sahihi hapo, najaribu kujiuliza alikuwa anamaanisha awachukuwe wabakaji alafu awapiganishe au? Hapana bado haiingii akilini...Nafikiri angeweka neno TUPINGE labda lingeleta maana zaidi.

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Edna! linaweza au aliweka kibao alikuwa ana maanisha tulipige vita:-)

Adela Dally Kavishe said...

mmh kweli kiswahili kigumu labda tupigane na ubakaji,

emu-three said...

Mhhh, hilo tangazo lipo hapa Bongo, na jamaa wa baraza la kiswahili hawajawahi kuliona?
Mhhh tutabakia kukisia kuwa alikuwa na maana gani aliyeandika hilo tangazo huenda alikuwa sio Mbongo(mswahili) na hakuna aliyemkosoa wakati ana-andika.
Kuna mzungu mmoja, tajiri alikuwa na kampuni yake, alikuwa anapenda kutukuzwa kweli na mara nyingi hujinadi na kusema, `mimi kwanza ni tya-ajiri, pili mimi ni msungu , tatu mimi ni bosi venu, kwahiyo sina makosa.
Basi akijikanayagakanayaga katika kuandika kiswahili au kuielezea, mkicheka, wewe...mtaipatapata,...nyinyi hamju kuwa mimi ni nyani(nani), naweza kuwafukiza (kuwafukuza)kazi. Mimi ni tajiri, musungu, na bosi venu...sasa mwacheka nyini...'basi kila akikasirika ndio anatupa mwanya wa kucheka zaidi na mwisho wake na yeye anaishia kucheka...Fikiria unamcheka mtu na yeye aanze kuwacheka, itakuwaje!

SIMON KITURURU said...

Labda liliandikwa na Mjerumani ambaye hakumalizia kozi ya KISWAHILI halafu mbahili!

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

ama: ubakaji wa watoto wadogo na wanawake wakubwa upiganishwe apatikane mshindi atakayepigana na ubakaji wa wanaume....lol!

Manake hapo ni Tupige vita ubakaji mwayego!

EDNA said...

Asante Yasinta,Adela,Emuthree umenchekesha na hiyo story ya mthungu.
KITURURU: Mjerumani alikuwa mbahili hahaaaa.
CHACHA: Tupiganishe alafu apatikane mshindi!!...Mweeeeeee kazi kwelikweli.

chib said...

Wabongo wengii ni wachemshaji, na wanaofanya kazi za uchoraji mabango wengi wao shule ilikuwa pilipili. Tembea tu maeneo ya Manzese midizini, mbagala charambe na hata pita barabara inayokatiza Tandale iwe kwa Tumbo, Bibi Nyau,... Jaribu kuangalia vibao vya matangazo, utasgaaa hichi kiswahili kilichoandikwa