Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday, 19 January 2011

DUNIA INA MAMBO!



ukistaajabu ya Musa utayaona ya filauni.....hebu soma hii habari mdau alafu tafakari kimya kimya....lol
Yule jamaa anayejiita Nabii Tito ameibuka na kioja cha kufungulia mwaka 2011.
Tito anayehubiri imani yenye ukakasi katika baa mbalimbali za Jiji la Dar es Salaam, hivi karibuni ametoa kijarida kinachoeleza kuwa ni ruksa kwa akina baba ambao ni waumini wa mahubiri yake ‘kulala’ na wafanyakazi wao wa ndani (mahausigeli).

Katika nukuu za kijarida hicho, Tito anatoa mfano kutoka Kitabu cha Mwanzo cha Biblia kuwa, Mtumishi wa Mungu Abraham alizaa mtoto wa kiume, Ishimaeli (Ismail) na kijakazi wake Ajili.

Aidha, katika kijarida hicho, Tito anasema kuwa akina baba kuwaacha mahausigeli wao ni dhambi mbele za Mungu na kusisitiza kwamba, lazima wapewe haki yao kama alivyofanya Abraham.

Kwa mujibu wa watu waliokisoma kijarida hicho anachouza shilingi za Kitanzania 1,000wamemponda Tito kwa mahubiri hayo kuwa ni ya upotoshaji huku wakitoa tahadhari kwamba akiachwa anaweza kuiharibu nchi.

Mwaka jana, Tito alitoa kijarida kingine kinachoruhusu watu kunywa pombe na wanaume kuoa mke zaidi ya mmoja, mahubiri hayo yalilaaniwa vikali na watu wanaomwamini Mungu.

Cha kushangaza mtu huyo hakukamatwa na badala yake anapeta kwenye mabaa akieneza mahubiri hayo yanayolaaniwa kila kukicha na viongozi wa dini.
Chanzo Global publishers.

10 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hakika huu sasa ni mwisho wa dunia jamani. Yamekuwa haya sasa hii inatisha tunakoenda ni kubaya tena kubaya kabisaaaa....

Simon Kitururu said...

Lakini haya mambo sio MAPYA sema tu Tanzania labda yanaanza kustukiwa siku hizi!:-(


BIBLIA kitabu cha ajabu sana na ndio maana kuanzia waliotaka UTUMWA uwe ruksa, WAAFRIKA KUSINI waliokuwa wanahalalisha APARTHEID waliotumia kitabu hicho kuhalalisha ,....


...na mengine mengi bila kusahau kwanini WATU kibao walikimbia UKATOLIKI na uzaliwaji wa makanisa kibao ya KIPROTESTANTI tokea enzi za akina Martin Luther au tu uzaliwaji wa mpaka USABATO na yote ni kwa kunukuu BIBLIA hiyohiyo.


DUNIA ina MAMBO na MAMBO YOTE kuna watu NI KAWAIDA na hushangaza tu kwa wale ambao hayo mambo hayafanani na maadili yao!


Na kwa bahati mbaya inasemekana MAADILI ni kitu cha kujifunza tu kwa asilimia kubwa.:-(

Rachel Siwa said...

Jamani huyo Tito mimi naona kama kajianzishia kadili kake kakupata pesa,kumbe hivyo vijarida vinampatia vijisenti na akienda bar pombe ananunuliwa kwa mgongo wa biblia.

Goodman Manyanya Phiri said...

Edna, Asante!!

Nimecheka sana na kuburudhika na haya mambo yaBongo pale niliposoma blogi yako hii mara ya kwanza kupitia ile ya Dada Yasinta kwa kuwa kweli hizo ni habari za kuvutia sana kwasisi tunayosoma mambo ya dini bila upendeleo; na haya mambo ya kuhubiri kwenye mabaa au sehemu za walevi yamevuma sana nchi nyingi duniani mfano Afrika Kusini na huko Australia: "WATAFUTE KONDOO PALE WALIPOPOTELEA"!



Lakini.....
“...Cha kushangaza mtu huyo hakukamatwa...”


Kwanini akamatwe, na mtu anatoa maoni au tafsiri yake ya Maandishi Takatifu? Si ndio uhuru huo ikiwa mtu hakusema "nendeni mkamwage damu" (au kitu kama hicho) ni haki yake kutoa maoni? Sindivyo dhehebu tofauti zilivyoanzishwa duniani? Watu wengi ni Wakrestu lakini hawajajisumbua hata kidogo kusoma historia na pale uKrestu ulikoanzia (hata kwenye imani potofu, mfano mambo ya umwagajidamu shaghalabagalaa au kikatili na panatisha kwelikweli) hadi hapo "ulipokamilika" kuwa Vitabu vya Biblia ya Kisasa.

Bila kulenga, nambieni, jamaani: wangapi wasomaji-blogi hii Wakrestu wamewahi kusoma kwa mfano vitabu vya APOCRYPHA wakati nayo APOCRYPHA ni sehemu moja yaBiblia ya hapo mwanzoni? http://www.google.com/search?hl=en&defl=en&q=define:apocrypha&sa=X&ei=Izc3TamaBMrssgbbwYinAQ&ved=0CBkQkAE

Goodman Manyanya Phiri said...
This comment has been removed by the author.
EDNA said...

SWAHILI NA WASWAHILI..GOODMAN MANYANYA PHIRI..karibuni sana kibarazani hapa.
Yasinta,Simon nimewapata.

Mzee wa Changamoto said...

Huyu anastahili kuitwa, awekwe PEMBENI kisha aulizwe ni nini hasa anataka.
Yaweza kuwa jambo dogo tu kama "kazi ya uhakika"
Ama MATIBABU YA AKILI.

Nawaza kwa sauti tuuuu!!!

Simon Kitururu said...

@Mzee wa CHANGAMOTO:

DUH! Kwanini unahisi anahitaji matibabu?
Na kazi ya uhakika ni ipi jamani hapa duniani?

Upepo Mwanana said...

Wahubiri wa uongo hao

emu-three said...

Mhhh, mimi hapa chichemi kitu, nawachikiliza nyie