Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday, 12 January 2011

Ha! Kumbe achumani ni mbwa!

Kuna jamaa mmoja alikwenda Mikoa ya Kusini, kwa bahati mbaya alichelewa usafiri na kufika usiku. Kwa vile Watanzania ni watu wa amani, aliamua kuomba msaada nyumba ya jirani ili kesho atafute wenyeji wake.

Alifika katika nyumba ya Mmakonde mmoja, alipobisha hodi, alikaribishwa vizuri sana. Bahati mbaya alikuta wamemaliza chakula, lakini mwenyeji wake alimueleza.

“Chamaani ngeni tumemalija chakula, lakini kipo chakula cha achumani (mbwa)”
“Kama kipo nipeni,” alisema bila kujua achumani ni mbwa, yeye alihisi ni Athumani mtu.

Aliletewa chakula cha mbwa na kukila chote, baada ya kunywa maji alimshukuru Mungu kisha akasema:
“Jamani mleteni Athumani nimshukuru.”

Baada ya muda lililetwa bonge la mbwa na kusimamishwa mbele yake.
“Haya chacha mchukuru achumani.”
“Huyu si mbwa?” Jamaa alishtuka.

“Ndiyo, ndiye achumani mwenyewe nchukuru chacha.”
Jamaa alitamani kutapika.

1 comments:

Yasinta Ngonyani said...

eeeh! jamani dhambi mweeh ila alishiba. Mie hakika nakuambia ningetapika mpaka nyongo!!!