Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday 6 April 2011

I`M TAKING YOU BACK INTO TIME.....


Milli Vanilli ni miongoni mwa wanamziki waliotamba sana miaka ya 80-90...Binafsi nilizipenda na nitaendelea kuzipenda nyimbo zako daima.
Moja wapo wa nyimbo zilizotamba enzi hizo ni huo hapo juu(Girl, I'm gonna Miss You.)
Wacha tukumbushie enzi hizo mdau.

6 comments:

Rachel Siwa said...

da Edna leo umewaza sana !!!!!!!umenikumbusha mnali sana wangu!!!!!Sipati picha ulikuwa unavaaje wakati huo wangu?

Simon Kitururu said...

Ilizingua sana ilivyokuja kugundulika waimbaji hawakuwa wao na wao kazi yao ilikuwa ni kuigiza tu kama wanaimba kwa kushika MAIKI/microphone wakati waimbaji wenyewe wanatengwa kisa sio wazuri wa sura .:-(

Music Business ina mambo yake ukifikiria akina Britney Spear nao siku hizi show zao wala hawaimbi live!:-(

Yasinta Ngonyani said...

Ni kibao kizuri kwali vya zamani ni vizuri...

EDNA said...

Rachael yaani wee acha tuu...Simon kumbe si wao wanaoimba hiyo sikuijua wangu.
Da Yasinta ni kweli vya zamani ni mbombiiii sana.

Simon Kitururu said...

Fab Morvan na Rob Pilatus ambao watu waliwadhania wanaimba walikuwa ni MAMODO tu UJERUMANI !

Kwenye BENDI walikuwa ni sura tu za kuuzia miziki . Ilikuwa wakati wa show inawekwa kaseti halafu wao wanajifanya kuimba.


Bendi hii alipoianzisha jamaa ajulikanaye kwa jina Frank Farian,.... ilikuwa na waimbaji
Charles Shaw, John Davis, Brad Howell, na wadada mapacha Jodie and Linda Rocco. Ila Frank Farian aliamini kuwa hawana muonekano wa kibiashara kimuziki na ndipo alipoamua kuwa show ifanyike kwa kutumia kasetti na LP na kuamua akina FAB na ROb watambulike kama Milli Vanilli .

Kwa hiyo MILLI VANILLI kama ilivyojulikana ilikuwa ni kitu kisicho halisi na ilikuwa ni njia ya kuwafanya watazamaji hasa MATINEJA waliohusudu NYIMBO za MAPENZI waamini wanaimbiwa na MAKAKA wawatamanio mamodo Fab Morvan na Rob Pilatus kwa kuwa muonekano wao kipindi kile ndio ulikuwa unapendwa hasa na WADADA ambao saa nyingine utamu wa MZIKI wa ALI KIBA hutegemea pia na wanavyozimia sura, KIFUA na six pack za ALI KIBA kimtamanio vinawatekenyaje.


Basi unajua tena siri ikabumbuluka tutokana na matatizo ya kaseti na LP /Santuri siku nyingine wakati wa show kunasa na kuanza kustua watu kuwa kitu sio live , pia waimbaji halisi kuanza kulalamika , ila kikubwa ni kwamba wakati wanapafomu live kwenye MTV wimbo-Girl You Know It's True ambao nao ulikuwa maarufu kuzingua kwa kuwa Santuri aka LP ilikuwa imekwaruzika na kuanza kurudiarudia live dunia ikiangalia kitu ambacho kikafanya ishindikane kuficha kuwa jamaa walikuwa sio waimbaji na kufanya wakanyang'nywa mpaka tuzo la Grammy walilopata.

Waimbaji halisi wakajaribu kufufua bendi kwa kuiita The Real Milli Vanilli lakini kama Frank Fabian alivyohisi tokea mwanzo na kuamua wasijulikane kama kazi ni yao wapenzi wa muziki hawakuwapenda .


Fab Morvan na Rob Pilatus walijaribu lakini kuimba wenyewe baadaye kabla Rob hajafa , ila uimbaji kwa bahati mbaya haikuwa talanta waliyopewa na MOLA.:-(


Haya maswala ya kuchagua SURA za waimbaji yapo sana lakini. LL Cool J alishawahi kushitakiwa kwa kutotaka muimbaji halisi wa wimbo wake ajulikane kisa ana sura mbaya. Na kwa mfano FINLAND kwenye miziki yao ya TANGO sura na muonekano ndio kiini. Kama mnene na unasura WAFINI wanaamini sio nzuri hata uimbe kama MALAIKA hushindi katika mashindano ya waimba TANGO.:-(


Musiki BIZINESS kiboko!:-(

emu-three said...

Umenikumbusha sana mbali ndugu yangu, wimbo huu unanikumbusha kipindi hicho nipo IDM-Mzumbe, napambana na semister...mambo yalikuwa magumu sana, sasa jiranii katika chumba cha pilii alikuwa na TV yake, siunajua tena watoto wa wakubwa, wanapewa kila kitu, kazi ni kusoma tu...nilikuwa nikiusikiliza huo mziki na huku najaribu kuandika mashairi yake...
Oh, nashukuru sana kwa kitu hicho!
Halloh, mkuu Simion, umetufunua macho kwa kitu ambacho kwakweli mimi sikuwa najua hivyo kabisa...loh, kweli bishara ni matangazo!