Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Monday, 18 April 2011

Vyuo Vikuu Afrika havitambuliwi.


Kuorodhesha vyuo vikuu kulingana na umaarufu ni desturi inayokua kwa kasi sana katika sekta ya elimu ya juu.

Orodha hiyo, inayojumuisha vyuo vikuu vilivyo maarufu zaidi duniani, ina walakini kwani bara zima halimo.

Hutapata hata chuo kimoja kutoka bara la Afrika kwenye orodha hiyo.

Vyuo vikuu vilivyoorodheshwa ni vya Marekani, Ulaya na baadhi kutoka China na Korea Kusini huku Afrika ikiwa imesahaulika.

Mazungumzo yanayohusu utandawazi wa vyuo vikuu yanatumia lugha ya kuvutia iliyorembwa kwa mada ya ushirikiano wa kimataifa, pamoja na mzunguko wa fedha katika mitandao ya kimataifa.

Ni rahisi sana kupotoshwa na mafanikio ya vyuo hivi ambavyo mazoea ni kuwatunukia watu tuzo na kujionyesha.

Swali ni, ikiwa ushindani wa kimataifa wa vyuo hivi utajikita katika hadhi na uwezo wa vyuo vichache, na hivyo basi bara zima likasahaulika, mambo yatakuwa vipi?

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni swali nzuri sana kwa kweli. Sijui ni kwa nini Afrika inasahaulika hivi?

Goodman Manyanya Phiri said...

Mambo yaliharibika pale tulipopoteza historia yetu nakuwapa wageni waandike. Baada ya hapo tukajaribu kuiga desturi zao. Mwisho hatuwezi kuhesabika kama watu wenye desturi zao kielimu; Afrika imeshakuwa kivuli tu cha Ulaya. Turudishe kwanza wenyewe heshima juu ya utamaduni na desturi zetu bila kuiga Wazungu ndipo ulimwengu utatuheshimu nasi!