Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, 24 May 2011

KISWAHILI.

Usahihi ni: Hapauzwi. Utatapeliwa.

Lipo tatizo kubwa kwa baadhi ya watu wa makabila fulani nchini Tanzania kuhusiana na matumizi ya herufi, 'R' na 'L' au 'H' na 'U' katika matamshi na hata kwenye maandishi. Pia, wapo wale ambao hushindwa kutofautisha kati ya herufi 'S' na 'Z' au 'P' na 'B' ama 'V' na 'F' na 'DH' na 'Z' na kadhalika.

Ingawaje kwa maneno mengine huwa si rahisi kupoteza maana kusudiwa, makosa hayo bado huweza kuleta maana tofauti kabisa na iliyokusudiwa, hasa kwa mgeni au mwanafunzi wa lugha ya Kiswahili.

Kwa mfano, neno 'ukiri' ni tofauti na neno 'ukili' au 'karamu' na 'kalamu'. Vile vile 'kazi' ni tofauti na 'kasi' kama ilivyo 'vuma' ikawa tofauti na 'fuma'. Kadhalika, 'barua' ni tofauti na 'parua' ama 'dhana' na 'zana'.

Matumizi yasiyo sahihi ya maneno hayo humlazimisha msomaji kujua maudhui ya habari kwanza ili kuweza kupata maana kusudiwa. Hii si vyema kwa wageni wanaojifunza lugha tunayojisifia kwayo kuwa ni asili yetu.
Credit to wavuti.

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Edna nashukuru nawe umegundua hili.

Goodman Manyanya Phiri said...

Wala sio tatizo la Kitanzania tu. Mzulu, Mxhosa na Mswati (ambae ni lugha ya mama yangu mzazi) wa hapa Afrika Kusini na Swaziland hana matumizi ya herufi "R". Na kama hakwenda shule kabisa utamwambia bure kwamba aina hii ya gari ni LORRY kwa Kiingereza na yeye atakwambia "LOLLY"!

Mara nyingi mimi huku kwetu naitwa "Pili" badala ya "Phiri", na huyo Mxhosa ukiona ameandika ukoo wake "Radebe", usidanganyike kutaamka kama unavyosoma kwani yeye anataamka "Khadebe"!


Kwa upande wa majirani zenu huko magharibi au niseme kusini mwa Tanzania, Wanyasa yaani....wengi kwao inakuwa kinyume. Kama vile kwao "L" hamna kabisa. Namkumbuka baba yangu mzazi na mzaliwa wa Malawi alijuwa sana Kiingereza.


Lakini kwangu mataamshi yake yalikuwa kama hivi: "RET ME TERR YOU, MY RAD: RAZINESS WIRR READ YOU TO COMPRETE FAIRURE AT SCHOOR, RIKE A BROODY FOOR!"


Hapo alikuwa na maana uvivu utanisababishia kushindwa mitihani yangu huko shuleni ("Let me tell you, my lad: laziness will lead you to complete failure at school, like a bloody fool")


Kabla hatujarekebisha mambo hayo; tujiulize: YANASABABISHWA NA NINI? NI MAZIWA YA MAMA ANAOMNYONYESHA MWANAE?

Mimi sijui kabisa lakini nimefurahi sana umelileta suali hili hadharani.

SIMON KITURURU said...

Mmmmh!

TITUS RICHARD said...

kweli inatudidi watanzania tubadilke kwani hivi ni sawa na kuua lugha yetu

TITUS RICHARD said...

DADA YETU HII NI KWELI KWA MAANA ITAPELEKEA KUFUTIKA AU KUPOTEA KWA SARUFI HUSIKA ZA KISWAHILI