Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday, 23 June 2011

JAMANI MADAKTARI MUWE MAKINI NA KAZI ZENU.


Hako kakijiti aliko kashika(Ove Sohlberg 65) kamemtesa kwa miaka 25.Kalisahaulika alipokuwa akifanyiwa upasuaji wa tumbo mwaka 1986,baada ya hapo tumbo lilikuwa likimsumbua mara kwa mara,Kila akienda hospitali madaktari walikuwa wakimwambia hawaoni tatizo lake.Mwaka huu ndio wamefanikiwa kukaona hako kakijiti na kukatoa.
Jamani huu tuuite usahaulifu au uzembe?

4 comments:

chib said...

Sijui ni kijiti cha nini na kilifikaje humo tumboni.
Tatizo la vitu vidogo aina ya miti, huwa havionekani kwa ufasaha kwenye vipimo vingi vya kawaida kama x-ray, ultrasound na hata CT Scan. Inabidi uwe na jicho na hisia kali kuweza kuhisi kama umeona kitu.
Polee zake kibabu huyoo

Swahili na Waswahili said...

Jamani yaleyale ya mguu na kichwa!Mungu ni mwema wamekiona na kukitoa.

SIMON KITURURU said...

Na nimesikia miezi hii ya summer kama uko Marekani kumbuka madaktari wanafunzi ndio yadaiwa huanza kufanya mazoezi ya udaktari kitu kifanyacho kuwa ,... unaweza kutibiwa na daktari mwanafunzi ambaye hakuelewa vizuri darasani . Yasemekana kipindi hiki cha summer ndio wagonjwa wengi Marekani hufa kwa uzembe wa madaktari hasa wale ambao kuna kitu inahitaji wafanyie zaidi mazoezi!:-(

emu-three said...

Kijiti? ingekuwa huku kwetu wangesema kautumia na `wataalamu wa mabo hayo'
Ila hawo watu waliofanya hivyo, sijui wafanyweje...jaribu kufikiria ndio wewe unaumwa, unaumwa...ukiendea hospitali unaambiwa huna tatizo na wengine wanahisi kuwa `unadeka'
Nakumbuka siku moja niliteguka kiuno, nikaenda hospitali moja kubwa mjini maeneo ya postaposta...kufika hapo hospitali ilikuwa mbinde...hayo maumivu...usiombe...nikawa najitahid sana ili watu wasinione ...siunajua tena, unajikaza kiume Nikamweleza docta ni wa `asili yake ni mueshia'
Akaniandikia dawa na sindano, halafu akaweka `C'.yaani kazini nisiende, nikapumzike...Sikuitaka hiyo `c' kwani ukiwa na C, kazini kwetu huna overtime.
Wakati natoka kwa yule docta nikaendelea kuhikaza kiume. Nikatibiwa , sasa wakati naondoka, nashangaa jamaa ananishika bega, akaniomba ile karatasi aliyoniandikia `c'
Akaniita ofisni kwake..akaifuta ile `c' kwa kashifa kubwa kuwa `siumwi' nasingizia ili nipate `c' anadai kuwa yeye katika uzoefu wake anajua nani anaumwa na nani haumwi! hebu fikiria wewe .,..hali niliyokuwa nayo...' Nilitamani MUngu atoe yale mateso ya maumivu yamwingie yeye ili aone raha yake!
Wengine tukipandwa na hasira hatuwezi kuongea, na ndivyo nilivyofanya nikamwambia `sahamani sana docta, kama nimekukosea, ila kweli mimi naumwa, na hata hivyo mimi sikuja hapa kwa ajiliya `c' nimekua kwa ajili ya matibabu...' nikaondoka!
Madocta mimi kama ni watu ninaowathamnini sana ni nyie na walimu...lakini wapo ambao badala ya kufanya kazi yao wanakuwa na chuki....wana unaguzi wanahisia za za kibanafsi...tuacheni hilo...udakitari ni wito na unatibu ujue unamsaidia mtu kutokana na madhila, uchungu fadhaa nk, wewe umeshikilia sehemu moja ya uhai wake...muogepeni sana mungu!