Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Sunday, 3 July 2011

HII NI KALI YA MWAKA!


AMA kweli duniani kuna mambo. Mwanamume wa India, Kailash Singh mwenye umri wa miaka 65, huenda akashika chati ya watu wanaotoa harufu mbaya za mwili na nywele, kwani kwa miaka 37 hajaoga wala kukata nywele na ndevu zake.

Sababu kubwa ya Singh kushindwa kufanya hivyo na nadhiri aliyokuwa ameiweka kwamba, ataoga, kukata nywele na kunyoa ndevu endapo atabahatika kupata mtoto wa kiume.

Kwa mara ya mwisho alikutana na maji kwa maana ya kuoga ilikuwa kabla ya sherehe ya harusi ya kumuoa mkewe, Kalavari Devi mwaka 1974.

Singh anaelezea sababu ya msimamo wake huo kuwa ni sharti la utabiri aliopewa na mmoja wa kiongozi wa dini ya Hindu kuwa atakapopata mtoto wa kiume, basi mtoto huyo atakuwa mwenye mafanikio makubwa sana kwenye maisha yake na atakuwa tajiri sana.

Ni miaka 37 imepita, lakini Singh anaendelea na msimamo wake wa kutooga mpaka pale atakapofanikiwa kupata mtoto wa kiume.

Sing ana jumla ya watoto saba wa kike, lakini juhudi zake zote za kupata mtoto wa kiume bado hazijazaa matunda.
SOMA ZAIDI
http://habarileo.co.tz/wikinyota/?n=18765

0 comments: