Tanzania imeongeza mgao wa umeme na kuufanya kuwa mkali zaidi kutokana na vyanzo vyake katika mabwawa ya umeme kupungua maji.
Mabwawa hayo yamepungua maji kwa kiwango kikubwa kutokana na ukame.
Lakini Shirika la Umeme Tanzania TANESCO limeahidi maeneo muhimu kama hospitali hayataariwa na mgao huo.
Afrika Mashariki inaripotiwa kuathiriwa na ukame mkali kwa miaka 60 iliyopita.
Watu wapato milioni 10 wanahitaji msaada wa chakula hasa nchini Somalia, Kenya na Ethiopia.
Tanzania inategemea zaidi ya nusu ya vyanzo vyake vya umeme kupitia mabwawa hayo.
Source BBC.
Monday, 18 July 2011
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comments:
Tatizo sugu da'Edna!
Post a Comment