Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Saturday, 7 April 2012

R.I.P STEVEN KANUMBA.

Yaani ni ngumu kuamini kuwa Kanumba ameaga dunia,nimetumiwa sms saa kumi namoja asubuhi kwamba Kanumba amefariki dunia,kwanza sikuamini nikafikiri ile siku ya wajinga bado inaendelea au naota.

Nilipowasha komputer na kuona kila blog ni rest in peace Kanumba ndio nikaamni hatunaye tena.Daima utakumbukwa na wasanii wenzako wote kwani wewe ni miongoni mwa wasanii wa tansia ya filamu walioleta mapinduzi kwenye movie za kibongo,na pia  watanzania wote kwa ujumla tutakukumbuka.Umeacha pengo ambalo kamwe haliwezi zibika.

Mchango wako kwa Taifa kamwe hautasahaulika kwani ulitengeneza ajira kwa vijana wengi ambao bila wewe huenda wasingekuwa pale walipo sasa.


REST IN PEACE KANUMBA WE WILL ALWAYS LOVE YOU AND MISS YOU.

1 comments:

Yasinta Ngonyani said...

pumzika kwa amani.Bwana alitoa bawana amechukua.