Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Saturday, 13 October 2012

Reactions: FUNGUA FIKRA MTANZANIA, UMASIKINI WETU NI FIKRA ZETU...!!!

Ni muda mchache umebaki kabla ya kufikia kilele cha kampeni ya miezi mitatu (3) ya Nchi Yangu , Wajibu Wangu UTAIFA KWANZA, changamoto ni nyingi sana tu lakini jambo moja lipo wazi kichwani mwangu, hili litafanyika, matembezi ya kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro, takribani 200km na zaidi, ikiwa ni uhamasisho na alama ya kuweka mbele maslahi yaTaifa letu kwanza, kutokuruhusu kutumiwa kwa maslahi ya wengine ama wachache, kuheshimu na kurudisha misingi ya maadili, heshima na dhamana ya uongozi na kubwa zaidi kubadilisha mtazamo wetu wa FIKRA, hatuhitaji kuwezeshwa, kusaidiwa, kudhalilishwa na mwisho wa siku rasilimali adimu za Taifa letu kuchukuliwa kwa jina la misaada ya wahisani, FUNGUA FIKRA MTANZANIA, UMASIKINI WETU NI FIKRA ZETU,

Nimebahatika kutembelea zaidi ya mikoa /kanda kumi (10) nimeonana, kuongea, kukutana na hata kufanya mahojiano na watoto mpaka waz, vijana hata vikongwe, watumiaji wa madawa haramu ya kulevya, watumiao miili yao, watoto waishio katika mazingira magumu, wanafunzi hata wafanyabiashara, TANZANIA ZAIDI YA UIJUAVYO,

Nimeweza kufanya mahojiano zaidi ya ishirini na vyombo mbalimbali vya habari (shukrani kubwa kwao), na nimekuwa nasisitiza ndugu zangu Watanzania, tuko tayari kuishi kwenye nyumba za vioo angali wenzetu wakiishi juu ya mawe? AMKA TANZANIA,

Nchi Yangu , Wajibu Wangu UTAIFA KWANZA
Matukio-Amani OleAfrika Aranyande M
Simu : +255 772 54 55 62
Barua Pepe : kwetutanzania@yahoo.com

0 comments: