Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday 25 October 2012

UCHAGUZI UVCCM.

  Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimkabidhi zawadi maalum Mwakilishi kutoka chama tawala cha  Zimbabwe Chipanga Kudzanai, kutambua mchango wa chama hicho kwa CCM, wakati wa Mkutano Mkuu wa nane wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) leo  Okt 23, mjini Dodoma.
 Mjumbe kutoka mkoa wa Mwanza, akipiga kura kuchagua Mwenyekiti, wakati wa Mkutano Mkuu wa UVCCM mjini Dodoma
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akicharaza gita zito la besi na bendi ya Vijana Jazz, wakati wa Mkutano Mkuu wa nane wa UVCCM kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere mkoani Dodoma.

 Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela akitoa utaratibu kabla ya kuanza uchaguzi mkuu wa jumuia hiyo leo mjini DodomkShamra shamra zikihanikiza kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere katika mkutano wa nane wa UVCCM mjini Dodoma.

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua mkutano Mkuu wa nane wa Umoja wa Vijana wa CCM mjini Dodoma leo.
Wagombea waliokuwa wanawania nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM. Kutoka kushoto, Lulu Abdalla Mshamu ambaye alijitoa wakati akijieleza kwa wajumbe,Khamis Sadifa Juma na Msaraka Rashid Simai ambao ndio waliochuana.

PICHA NA HABARI NIMETUMIWA NA ADAM MZEE.

0 comments: