Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Sunday, 17 February 2013

BREAKING NEWS: PADRE EVARISTUS MUSHI AMEUAWA KWA KUPIGWA RISASI ZANZIBAR...!!!

 
Padre E. Mushi Paroko wa parokia ya Minara Miwili Zanzibar ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika asubuhi hii. 

Ameuawa wakati akijiandaa kuingia kanisani akitokea kwenye gari yake ambapo ghafla ilitokea gari ndogo na waliokuwamo ndani ya gari ile wakamrushia risasi. Kwa siku za hivi karibuni kumekuwako na vitisho vya wazi wazi dhidi ya wakristu huko visiwani Zanzibar ambapo inaelezwa kuwa jeshi la polisi halijafanya juhudi yoyote kuzuia tishio hili. Kumekuwapo na vipeperushi vinavyodai kuwa kupigwa risasi kwa padre Ambrose sio mwisho wa mapambano.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA IEPUSHE NA MACHAFUKO YANAYOTOKEA KILA KUKICHA.

0 comments: