Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday, 9 May 2013

BONGO DAR ES SALAAM ISIYOISHIWA NA VITUKO,TUMEZOEA KUSIKIA NA KUONA MUME/MKE KUFUMANIANA LAKINI HII YA SASA BALAA.

Aibu hiyo ya mwaka ambayo ilionekana pia kama kituko ilijiri Mei 3, 
mwaka huu ndani ya gesti moja maarufu iliyopo 
Devi’s Corner –Tandika, jijini Dar es Salaam.
Mama Salome akimpa kisago mumewe baada yakumfumania 
akiwa na 
 Mwita (kushoto) anayedaiwa kuwa shoga

...Watuhumiwa wakipelekwa kituo cha polisi.

Baba Salome (kulia) na Julius Mwita baada ya kufumaniwa wakiwa
 katika hatua za mwisho za kuingiliana kimwili.

Aibu hiyo ya mwaka ambayo ilionekana pia kama kituko ilijiri Mei 3, mwaka 
huu ndani ya gesti moja maarufu iliyopo Devi’s Corner –Tandika, jijini 
Dar es Salaam.
HABARI ZA AWALI
 
Awali ilidaiwa kuwa, mwanaume huyo na baba Salome mwenye mke na 
watoto wawili wanaomtegemea kwa kila kitu, walionekana wakiingia 
kwenye gesti moja ambayo pia ipo maeneo hayo hali iliyozua maswali kwa watu waliokuwa wakiwafahamu.
“Unajua tatizo lilianzia wapi? Baba Salome na yule mwanaume mwenzake 
walionekana wakiingia gesti moja kisha wakatoka, wakaingia nyingine
 pia wakatoka, ndipo watu wanaowafahamu wakajiuliza kulikoni wawili 
hao kutembelea gesti siku hiyo, wakawafuatilia,” alisema mnyetishaji mmoja.
 
Akaendelea: Lakini watu waliwafahamu kwa namna mbili tofauti, 
baba Salome ni mtulivu, mwadilifu, mwenzake watu wanasema 
ana ‘katabia’ ka kutaka kuwa faragha na  wanaume wenzake 
bila kujulikana nini anakitaka katika usiri huo.
Madai zaidi yakawekwa wazi kwamba, baadhi ya watu walikwenda 
kwenye gesti walizokwenda wawili hao na kuulizia nini walikuwa 
wanakitaka, ndipo siri ikawekwa wazi kwamba wanatafuta chumba 
cha kupumzika kwa siku hiyo lakini kwa sheria za Jiji la 
Dar es Salaam (kama siyo za nchi nzima), wanaume wawili 
hawaruhusiwi kulala chumba kimoja. Chanzo kikasema: 
Wambeya wakawaona wakiingia kwenye gesti ya tukio, 
wakapewa chumba. Ndipo wakakimbia nyumbani kwa 
baba Salome na kumtonya mkewe, mama Salome kwamba 
mumewe ameingia gesti.
MAMA SALOME AJA JUU, AMTAJA KIDAWA
 
Kichekesho zaidi kinaangushwa kwamba, baada ya kuambiwa 
mumewe amezama gesti, mama Salome ambaye ndiyo kwanza 
alikuwa amefika kutoka  kwenye mikopo ya Finca, alitoka 
mbio huku akisema anakwenda kumtoa sikio la kulia Kidawa 
akiamini mumewe ameingia gesti na mwanamke huyo.
“Watu walimwambia mumewe hakuingia gesti na Kidawa 
bali mwanaume mwenzake. Kwanza mama Salome aliomba
 asitaniwe juu ya hilo, lakini akasisitiziwa,” alisema mtoa habari huyo.
NJE YA GESTI, MAMA SALOME AFUNGUKA
 
Akizungumza kwa jazba na waandishi wetu nje ya gesti hiyo, 
mama Salome alisema kwamba alipata taarifa siku nyingi 
mumewe ana ukaribu na mwanaume huyo ambaye mitaani watu 
wanasema  anajihusisha na vitendo vya ushoga. “Nilipozipata 
taarifa hizi sikuziamini, nilidhani ni Kidawa ndiyo kaingia gesti 
na mume wangu, maana Kidawa ndiye mbaya wangu,” alisema 
mwanamke huyo kisha akazama ndani ya gesti akiwa na polisi 
ambao haikujulikana walikotokea.
FUMANIZI TAAP!
 
Huku mumewe na mwanaume mwenzake wakiwa hawana hili 
wala lile kule chumbani, mlango ulisukumwa na kufunguka 
ambapo mwanamke huyo aliwakuta wawili hao wakiwa 
wameshavua baadhi ya nguo. Wote walishtuka kuona wameingiliwa!
 
“Yaani roho inauma sana, sijui ni kitu gani umekosa 
kwangu mpaka unakuja kwa mwanaume mwenzako jamani 
 baba Salome,” alisema huku akilia mama Salome.
MWANAUME MMOJA AANGUA KILIO
 
Baada ya kugundua wamenaswa, mwanamke aliyekuwa na 
baba Salome aliangua kilio huku  akiomba kusamehewa kwa vile 
yeye ni mume wa mtu, lakini kilio chake hakikusikika kwa polisi 
 ambapo waliwafunga pingu na kuwataka kuelekea katika kituo cha polisi.
MMOJA ALIA NA MAPAPARAZI
 
Wakati wakitoa maelezo kwenye kituo cha polisi, mwanaume aliyekuwa 
na baba Salome alijitambulisha kwa jina la  Julius Mwita, mkazi wa 
Devi’s Corner ana  mke na watoto wawili na aliwaomba sana 
mapaparazi wamhifadhi kwani wakwe zake wakimuona ‘itakula  kwake’.
 
“Jamani mapaparazi nipo tayari kwa lolote naomba sana tuyamalize 
hapahapa, mimi ni mume wa mtu, wakwe zangu wananiheshimu
 na kunithamini sana,” alisema Mwita.  
Hata hivyo, pamoja na kilio hicho mwanaume huyo aliishia 

kuswekwa lupango na baadaye kuhamishiwa katika Kituo 
cha Polisi cha Chang’ombe kwa hatua zaidi.

2 comments:

emu-three said...

Hata watoka bara nao wamo, mbona dunia imeguka kubaya. Nafikiri sasa shetani anatushangaa, maana tumemzidi yeye kwa maasi. Mungu tuepushia na balaa hili

EDNA said...

Hahaaa kweli tumemzidi hata shetani kwa mabalaa.Hao niwachache waliobambambwa hatujui wako wangapi wanaofanya uozo huo mmmmh.