Jumatano wiki hii, jarida maarufu
na kongwe duniani la TIME, lilimtangaza kiongozi wa kanisa Katoliki duniani
Papa Francis, kuwa mtu aliyekuwa na ushawishi mkubwa kwa mwaka huu wa 2013.
Tuzo hiyo, ijulikanayo kama PERSON
OF THE YEAR, hutolewa kwa mtu ambaye ametawala vyombo vya habari kwa mwaka
husika, iwe ni kwa mambo mema ama mabaya.
Mwaka jana, Rais Barak Obama alishinda tuzo hiyo kwa kutetea kiti chake cha urais nchini Marekani.
Na katika fainali ya tuzo za mwaka
huu, walikuwemo pia Rais wa Syria Bashar al Assad ambaye amekuwa akituhumiwa
kutumia gesi ya sumu kuua raia wake, pia mwanasayansi aliyevujisha siri za
serikali ya Marekani Edward Snownden, Rais Obama na wengine sita.Hii ilikuwa ripoti ya Disemba 14, 2013
Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
0 comments:
Post a Comment