Monday, 30 November 2009
HIVI NI KWELI BABU SEYA NA WATOTO WAKE WALIBAKA?
leo ilikuwa ni siku ya kusikiliza rufaa ya Babu Seya na watoto wake watatu.Papii Nguza, Nguza Mbangu na Francis Nguza.Babu Seya na watoto wake wanapinga kifungo cha maisha walichohukumiwa na mahakama ya hakimu mkazi kisutu.Babu Seya na watoto wake walihukumiwa kifungo hicho mwaka 2004, baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa katika kesi iliyokuwa ikiwakabili ya kudhalilisha kijinsia watoto wa kike, ilitolewa na Hakimu Bi. Addy Lyamuya, ambaye kwa sasa amestaafu kazi.
Maombi ya rufaa yaliyowasilishwa na aliyekuwa wakiliwa wa Babu Seya, Bw. Hubert Nyange, ambaye sasa amejitoa yanaonesha sababu 15 za kupinga adhabu hiyo, ikiwamo kwa nini Jaji wa Mahakama Kuu hakuona kuwa hakimu aliyesikiliza kesi hiyo alishindwa kutokuwa na upande na kuathiriwa na mtazamo hasi juu ya wateja wake.
Babu Seya na watoto wake walikata rufaa Mahakama ya Rufaa baada ya Mahakama Kuu chini ya Jaji Thomas Mihayo, kutupilia mbali rufaa yao.
Nguza na watoto wake watatu walihukumiwa adhabu hiyo kwa kuwadhalilisha kijinsia wanafunzi wa kike maeneo ya Sinza, Dar es Salaam.
Swali ni je ni kweli Babu Seya na watoto wake walibaka? na kama si kweli haki iko wapi?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment