Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Friday, 6 November 2009

MALEZI YA WATOTO YAZINGATIE VIPAJI KUCHOCHEA MAENDELEO

Uwezo wa vijana wengi nchini Tanzania ni mdogo katika kukabiliana na changamoto za maisha na ushindani kutoka kwa vijana wa mataifa mengine Duniani.Ambapo akili zao zimedumazwa na malezi,elimu duni, pamoja na makuzi wanayopewa katika familia.Ongezeko la vijana wasiokuwa na ajira,matukio ya uhalifu,umasikini wa kipato na maendeleo duni katika taifa lenye rasilimali na hazina kubwa ya madini,linachangiwa na malezi yasiyothamini vipaji vya vijana husika.Wazazi wengi nchini wamekuwa na utamaduni wa kuwazuia watoto wao kuendeleza vipaji walivyonavyo, na kuwataka wawe warithi wa shuguli zao.Inashangaza kuona maisha ya vijana walio wengi ni duni wakati wanaishi katika nchi yenye utajiri wa kila aina kwa maana ya rasilimali,vitu kama madini, maziwa,mito,mbuga za wanyama,milima na ardhi yenye rutuba.Naamini wengi wetu tunajiuliza maswali mengi juu ya ufukara uliopo nchini,wakati Taifa lina rasilimali ambazo hazipatikani nchi nyingine yoyote Duniani.
Toauti ya maisha imezidi kuwa kubwa ambapo kundi la masikini ni vijana linaongezeka kwa kasi, vifo vya watoto,wanawake.Ongezeko la wangonjwa na huduma duni za kijamii zimeendelea kuwa za kudumu katika nchi.
Katika mazingira hayo wimbi la wageni kutoka mataifa mengine kwa kivuli cha uwekezaji wamezidi kuongezeka,na kuchuma matunda ya nchi kwa kutumia mianya iliyopo kwa manufaa ya nchi zao,wakati wazawa wakiangalia bila kujua wafanye nini,zaidi ya kumuomba Mungu ili aweze kuwaokoa.

0 comments: