Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Friday, 4 December 2009

AFRICA KUWA NA MSIMAMO MMOJA COPENHAGEN

NCHI za Afrika zimetakiwa kuwa na msimamo mmoja kabla ya kufanyika kwa Mkutano wa Mabadiliko ya Tabia Nchi, Copenhagen, Denmark wiki mbili zijazo ili kuzibana nchi tajiri zinazochafua hali ya hewa.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt. Batilda Burian wakati akifungua mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi Dar es Salaam.

Alisema kuwa nchi za Afrika zinatakiwa ziwe na msimamo mmoja ili ziweze kubana nchi tajiri zinazozalisha hewa ya ukaa kabla ya mkutano mkutano huo.

"Ili kukabilina na hali hii ya mabadiliko ya tabia nchi wananchi pamoja na jamii wanatakiwa kutunza mazingira kwa kupanda miti na kuacha kufugo mifugo mingi kupita kiasi katika eneo," alisema Dkt Burian.

Alisema kuwa tayari serikali imeshapokea dola za Marekani milioni 3.5 kwa ajili ya kujenga ukuta wa Mto Pangani na wakazi wa Pwani walioathiriwa na maji ya chumvi yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Pia alisema wamepokea dola za Marekani milioni 3 kutoka Japani kusaidia meneo ya Longido, Pwani na Njombe kukabilina na tatizo hilo.

Alisema Euro mili. 2.2 zitasaidia kujenga vituo katika vijiji sita Tanzania Bara na visiwani ili wananchi waweze kupatiwa elimu jinsi ya kutunza mazingira na kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa.
(Source Majira)

0 comments: