Monday, 28 December 2009
MAKONGO HKL 2004 MPOOO!!!
I wish i could turn back time,Hii inanikumbusha mbali enzi hizo tupo Makongo High school HKL nakumbuka ilikuwa kama wiki moja tuu baada ya kuanza form five, mwalimu mmoja tulikuwa tukimuuta Cordinator alikuja darasani kwetu akakuta tunapiga kelele cha ajabu alitusimamisha watu wawili tuuu mimi na Neema Minja eti ndio aliotuona tukipiga kelele,tukaambiwa tuandike barua ya maelezo kwa nini tunapiga kelele? masikini wa Mungu hatakuandika hiyo barua ya maelezo tulikuwa hatujui tukamuomba atusamehe akakataa,basi tukajijengea uadui na huyo mwalimu baada ya kipindi fulani akawa rafiki yetu akiniona mimi atauliza Neema yuko wapi akimuona Neema atamuuliza pia.
Darasa letu lilikuwa na sifa ya kila aina,kikibwa tuliishi kama ndugu mtu akiwa na Birthday yake tulisherehekea darasani,nakumbuka HGL walikuwa wakitusema eti tunapenda kuparty,kuchelewa shule ilikuwa kawida yetu kusinzia darasani ndo usiseme,kwa kelele tuliongoza,Adhabu kwetu ilikuwa kitu cha kawaida,tulibebeshwa madumu,tulichimba mashimo kwa sana tuu na Marehemu Afande Miraji.
Nakumbuka Marehemu Miraji alishawahi kutupa laana kwamba HKL wote tutafeli hahahaa laana yake ilikuwa baraka kwani wote tulifaulu wote unawaona hapo juu wako vyuo vikuu na wengine washamaliza.
Darasa letu lilikuwa na watu wa kila aina,siku moja tukaamua kufanya party na kuwa pa zawadi watu kutokana na sifa zao,tulianza na
The best MROPOKAJI: hii ilienda kwa Khamar Kashoro huyu bwana alishahi kumropokea mwalimu wa history kuwa hajui history yeye ndiye anayejua.
Ya pili ilikwenda kwa The best MCHELEWAJI: hii ilikwenda kwa watu 3 JITIHADA,JAMILAH na mkaka mwingine nimemsahau jina, hawa bwana walikuwa wakija muda wanaotaka wao.
Ya tatu ilikwenda kwa the best MSINZIAJI,Hii walinipa mimi Reheme na swalehe sisi bwana mwalimu akiingia tuu na usingizi nao unaanza.
Ya mwisho ilikwenda kwa the Best Mtoro,hii ilikwenda kwa Edson yeye bwana anaweza akakaa hata mwezi asionekane shule chaa ajabu kwenye attendance alionekana yupo kila siku kwani mimi ndiye niliyekuwanashika daftari ya attendance kila mtu nilikuwa na tiki yupo hata kama hajaonekana mwezi sikuwa na hiyana.Party zote zilikuwa zikiandaliwa na kaka mmoja aitwaye Sunbella yeye bwana vikimujia kichwani tuu anatangaza party.Mwisho nawatakia Heri ya mwaka mpya 2010 popote pale mlipo.LOVE YOU ALL.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Imenifurahisha sana hii post.
Hii post hata kama huwajui hawa watu. unajikuta unacheka mwenyewe kwa jinsi ilivyoandikwa kwa mbwembwe.. Asante sana Edna.. www.greatdesign.co.tz
Post a Comment