Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday, 27 January 2010

Bongo Inazidi Kung`ara!!


So far so good, bongo Yetu inazidi kung`ara na majengo Mapya, jengo hili lipo katika makutano ya morocco ambako zamani kulikuwa na jengo la Gogo hotel.Inapendeza kwa kweli.Picha kwa hisani ya Ray The Greatest.

5 comments:

Anonymous said...

hilo ni jengo ambalo ndio litakuwa makao makuu ya kampuni ya simu Zain

Mdau
Haninge

EDNA said...

Asante kwa taarifa Mdau wa Haninge, hata nilikuwa sijui

Yasinta Ngonyani said...

kumbe hata mie nilikuwa sijui hii habari. Na Da Edna ni kweli Bongo inazidi kungára ngára...

Mzee wa Changamoto said...

Tatizo ni kuwa mng'aro huu uko juu na haujali yaliyo chini.
Bongo inang'aa kwa majengo lakini hawarekebishi mifumo ya majitaka. Sijui haya majengo yote yanaungwa kwenye mabomba gani ya kupeleka uchafu?
Bongo inang'aa kwa "vikwangua anga" lakini hawaongezo uzalishaji wa maji safi. Matokeo yake maji yanapatikana masaa 2 ama moja kwa siku.
Bongo inaongeza maghorofa lakini hakuna anayepanua barabara, kuongeza daladala wala kufikiria sehemu za maegesho.
Nadhani BONGO INAZIDI KUNG'AA KWA KUWA INAPAKWA MAFUTA BILA KUOSHWA.
Siku ikija kugundulika kuwa wanatumia mifumo ya majitaka ya miaka ya mkoloni, ndio watakapojifunza kuwa Dar imekalia bomula vinyesi na mikojo.
Ikizibaaaaaaaaaaaaaa!!!!
Tutawaona CNN wakiogelea "makimbani"

http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/09/tanzania-yangu-ijengayo-ghorofa-bila.html

EDNA said...

Nakubaliana na wewe mzee wa changamoto asilimia zote,wanajenga majengo mazuri yenye kuvutia lakini utakuta hakuna parking....hiyo ndiyo Bongo bwana mambo ni shaghala bagala.