Jeshi la Nigeria limesema limechukua udhibiti wa mji wa Jos,ambapo mapigano ya hivi karibuni kati ya waislamu na wakristo yalisababisha vifo vya watu kadhaa.
Luteni Kanali Shekari Galadima ameiambia BBC kuwa mji "uko shwari" wakati jeshi likihakikisha kuwa amri ya kutotoka nje kwa muda wa saa 24 inatekelezwa. Amesisitiza kuwa hakutakuwa na ghasia tena.
Lakini mwandishi wa BBC katika eneo hilo anasema ghasia sasa zimezidi hadi katika mji wa Pankshin, kilomita 100 kutoka Jos.
Makundi ya kutetea haki za binaadamu yanasema takriban watu 200 wanaaminika kufariki dunia tangu Jumapili.
Mji wa Jos umekumbwa na mapigano ya kidini kwa takriban muongo mmoja uliopita.
Chanzo BBC.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
Dada naona umetoa ile Picha yako Nzuri, mimi nilikuwa nafungua blog yako kuagalia tuu jinsi ulivyo jaliwa macho
Mdau
Haninge
usijali nitaweka nyingine!
Kuna sehemu nyingine matatizo ndio sehemu ya maisha. Huyo mdudu wa ghasia Nigeria sijui ataisha lini?
Post a Comment