Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Saturday, 30 January 2010

Mke wa waziri wa Afrika Kusini akamatwa!

Mke wa waziri wa masuala ya kijasusi wa Afrika Kusini amekamatwa kwa madai ya kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.
Sheryl Cwele, mwenye umri wa miaka 50, mke wa Siyabonga Cwele, amefikishwa mahakamani akishtakiwa kwa jaribio la kuingiza cocaine nchini Afrika Kusini.

Bi Cwele ameshtakiwa kwa kumtumia mwanamke mmoja kuchukua dawa hizo Uturuki na kumwajiri mwanamke mwengine kuzichukua kutoka Brazil.

Amewekwa rumande mpaka dhamana yake itakaposikilizwa katika wiki moja ijayo.

Bi Cwele anakabiliwa na shutuma hizo pamoja na Frank Nabolis, raia wa Nigeria aliyekamatwa Afrika Kusini mwezi Desemba.

1 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Ni nani ambaye hajui kwamba biashara hizi ni za wakubwa?