Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Saturday, 2 January 2010

Mshukiwa wa Al-Shabab ajeruhiwa Denmark

Polisi nchini Denmark wamempiga risasi na kumjeruhi Msomali kwenye nyumba ya mchora katuni aliyechora katuni zenye utata za Mtume Mohammed.
Polisi wamesema mtu huyo ambaye ana uhusiano wa karibu na kundi la kiislam nchini Somalia la Al-Shabab, ameingia nyumbani kwa Kurt Westergaard katika mji wa Aarhus, akiwa amejihami kwa kisu na kutishia kumwua mchora katuni huyo.

Polisi walidokezwa tukio hilo kupitia ala za electroniki zinazotoa ishara ya hatari, na kisha kumpiga risasi mtu huyo mara mbili.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa anashukiwa kuhusika na vitendo vya kigaidi katika nchi za pembe ya Afrika.

Bw Westergaard amepokea vitisho kadhaa vya kumwua tangu kuchapisha katuni hizo kwenye gazeti miaka minne iliyopita, ambazo Waisamu wengi walizichukulia kama fedheha na kejeli ya imani yao.

5 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Sijawahi kufanya kejeli na imani ya mtu na nadhani mchoraji alipaswa kuwa makini alipochora ile katuni.
Hata hivyo siamini kama fedheha ya katuni inaweza kumtuma mtu kumuua mchoraji kwa kisingizio cha kusimamia imani.
Imani inasisitiza KUSAMEHE.Na hapo ndipo kilipo KIPIMO na UGUMU wake. Kuwa tunapokwazwa twahitaji kusamehe na unavyoweza KUSAMEHE unapokwazwa na kubwa zaidi ndivyo unavyohidhihirisha ukomavu wako kiimani.
Kwa hiyo kwa mtazamo wa imani HATUTAKIWI KULIPIZA KISASI kwani kwa namna tunavyoweza kuwasamehe, kuwavumilia na kuwaombea watukwazao, ndivyo tunavyojengeka kiIMANI.
Blessings

Yasinta Ngonyani said...

Nimepita kukusalimia nimekuona sehemu karibu sana.

EDNA said...

Mzee wa Changamoto kumbuka kuwa binadamu tumetofautiana kifikra unaloliona wewe ni heri mwingine analitazama katika mtazamo tofauti.Wengine hawahujui kama kuna kitu kinaitwa kusamehe.
Dada YASINTA nimepokea salam zako, nami nakukaribisha kwa Moyo Mkunjufu.
Amani ya Bwana Yesu iwe nanyi

Mzee wa Changamoto said...

Najua Da Edna.
Ndio maana naamini THE WAY YOU SEE THE PROBLEM IS THE PROBLEM

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Imani zingine bwana, bora kkukua kiroho. wanauana kulinda imani ambazo hata waanzilishi wake hawazitamani tena

labda ni kuppoteza matumaini maishani wakuu