Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Monday, 4 January 2010

Rais Zuma Kuoa Mke wa Tano!


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma atafunga ndoa ya tano baadaye leo.
Harusi yake itafanyika kuzingatia mila na desturi za jamii ya Zulu ambapo Thobeka Stacey Mabhija atakuwa mke wa tatu wa Zuma.

Wake wengine wawili wa Zuma Sizakele Khumalo-Zuma na Nompumelelo Ntuli-Zuma sharti washiriki sherehe ya leo ili kumkubali mke mwenza wao.

Rais Zuma pia amesha mposa mwanamke mwingine na tayari amelipa mahari.

Waandishi habari wamesema imani ya Zuma kuwa na wake wengi imeigawanya jamii Afrika Kusini.

Baadhi wanamuunga mkono huku vijana wengi wakisema desturi hiyo imepitwa na wakati.

Mmoja wa wake wa Zuma Kate Mantsho-Zuma alifariki dunia na rais huyo alitengana na waziri wa mambo ya ndani wa Nkosazana Dlamini Zuma.

2 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Anadumisha mila na utamaduni wa Mwafrika huyu. Kuna nini cha kushangaza hapa? Waisilamu wakioa wake wengi mbona hatushangai?

Kule Usukumani (na naamini pia katika makabila mengi) bado ni rukhsa kuoa wake wengi na kijijini kwetu kuna jamaa wenye wake wawili, watatu, wanne, watano na hata sita.

Hata hao wasio na wake wengi - wana nyumba ndogo Ilala, Temeke na Kinondoni? Si ni kitu kile kile tu au?

John Mwaipopo said...

kama alivyosema masangu. hizo ni mila zao sie hazituhusu. ingawaje hata sie tumebadilishwa na ukristo. tukaukubali ukristo, tukaamua kumuonyesha mke mmoja kanisani na kuwaficha wengine wasio na idadi kwa jina la nyumba ndogo.