Wednesday, 10 February 2010
Soda Increases Risk Of Cancer!
Do you drink much soda like me? Stop it.... New research shows that soft drinks may cause cancer.So wale wenzangu na mimi hii si habari njema kabisaaa!tuanze rasmi kunywa maji mengi kuliko soda.
American scientists have made study, suggests that consumption of soft drinks increases the risk of cancer. A few years ago made a similar study in Sweden, where the researchers came to the same result.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
4 comments:
Nshukuru silazimiki kuacha kunywa soda kwani situmii kabisa. Pia Edna asante kwa habari hii .
Hongera kama si mnywaji wa soda Da Yasinta,maana mimi nakunywa kama chai lakini baada ya habari hii naacha kabisa.
Ukiwasikiliza vizuri wanasayansi na tafiti zao unaweza ukashindwa kuishi kwani inayoonekana karibu kila kitu kinasababisha kansa, shinikizo la damu na magonjwa mengine. Mimi huwa wananichangaya pale wanapotoa sababu zinazokinzana. Leo watasema kahawa inaongeza shinikizo la damu na upataji wa aina fulani za saratani, na kesho tena kahawa hiyo hiyo itaonekana kuzuia kansa fulani na hata dementia. Bia utaambiwa zinaleta kansa ya matumbo na wakati huo huo zinazuia baadhi ya kansa. Wine inazuia kansa na kushusha shinikizo la damu lakini pia inaongeza upataji wa kansa ya matiti kwa akina mama....Mbaya zaidi, huwa hawasemi nini cha kufanya wakati mambo yanapogongana namna hii. Mimi huwa nawasikiliza kwenye vitu ambavyo vimejulikana havina faida kabisa kabisa kama sigara. Vinginevyo utashindwa kuishi au pengine itabidi kula asali na nzige tu kama Yohana Mbatizaji!
Hata ukiacha kunywa soda, bado kuna vyakula na vinywaji vingi sana vinayoweza kukuua.
Pengine hili limefumwa katika falsafa yangu ya maisha. Kwani maisha hasa ni nini jamani? Hata ukiongeza miaka miwili katika maisha yako kwa kuacha kunywa soda (japo pengine hili ndilo jambo likupalo furaha katika maisha yako) itakusaidia nini?
Tembelea blogu ya http://kona-ya-afya.blogspot.com/ uone ninachokisema hapa. Karibu kila kitu kinakatazwa!
Mimi ninakunywa soda mara moja moja!
afadhali sasa kuanza kunywa TOGWA atleast sijawahi kusikia kuwa togwa ni mbaya....lol
Post a Comment