Watoto ni viumbe wadadisi ambao hupenda kujua kila wakionacho, kwa wale wenye watoto au wale wenye ukaribu sana na watoto watakubaliana na mimi....Jana nikiwa kwenye Train naelekea nyumbani nilikutana na habari hii ambayo nimeona niwashilikishe.
Kwenye train kulikuwa na mama na baba pamoja na watoto wao wawili, wakike ana miaka kama mitatu hivi na wakiume mwaka mmoja, ndani ya train kulikuwa kimyaaaa basi yule mtoto mkubwa akavunja ule ukimya kwa kuumuliza mama yake, Mama mimi na Erik tutaoana lini? yaani Erik kaka yake, watu wote waligeuka kumuangalia yule mtoto kila mtu alitabasamu, mama akajibu hamuwezi kuoana kwa sababu Erik ni kaka yako, kale katoto kakanyamaza kwa sekunde kadhaa ghafla kakasema basi nitaoana na baba kwa sababu baba sio kaka yangu, Mama akasema huyo ni baba yako huwezi kuoana naye.
Yule mtoto akamtaja mtu mwingine kwa jina la Johnson sasa sijui huyo Johnson ana umri gani? akasema huyo ndiye atakaye olewanaye, mama akaguna mmmmh kisha mama akamwambia yule mtoto, wewe bado mtoto ukikuwa ndio utaolewa.... mtoto akajibu kwani nitakuwa lini?
Bahati mbaya nikashuka kituo kilichofuata kwa hiyo sijui nini kiliendelea. Kwa ujumla nilijifunza mengi kutoka kwa yule mtoto, ni mengi watoto wanayaona na kuyasikia na wanatamani ufumbuzi wake lakini hawapewi ufumbuzi labda kutokana na Umri wao.....Ungekuwa wewe ndio mama wa huyo mtoto ungejibu nini?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
4 comments:
Edna nwe.... ok nadhani ningejibu kama huyo mama. Kwa kweli watoto ni wadadisi kazi tunayo...
Watoto wadadisi kwa bahati mbaya watu wengi tumefunzwa KUWADANGANYA.
Mimi naona mama ya huyo mtoto alikuwa anapatia majibu lakini.
sina jibu ningejibu nini ila kama ingekuwa huku kwetu nadhani angekula KWENZI za haja...lol
Hhaaa, Chacha umpige kwenzi na yeye anataka kujua jamani. Kitururu ni kweli wazazi huwa hawawaambii ukweli watoto wao wanapouliza.
Post a Comment