Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Monday, 12 April 2010

MUNGU NA ASHUKURIWE KWA KILA JAMBO!

Unawakumbuka hawa mapacha walioungana? sasa wamekuwa wakubwa na warembo zaidi. Mungu ni wa ajabu hatuna budi kumshukuru kwa kila jambo atutendealo.
Mapacha wakiwa katika nyuso za furaha,

Picha ikionyesha sehemu za mwili walizoungana.


4 comments:

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

nikitaka kuoa ntamuoa yupi kati ya hao?

Kama ni wote wakizaa mtoto atakuwa wa nani ama nani atasikia uchungu zaidi ya mwingine?

Ama kweli hujafa hujaumbika na Mungu ashukurie kwa kila jambo!

EDNA said...

Chacha unaooa wote,mtoto atakuwa wa wote.Nahisi na uchungu watasikia wote.....kweli hujafa hujaumbika.

Yasinta Ngonyani said...

Ama kweli Mungu wa ajabu. Jana nilipokuwa kazini nilikuwa naangalia TV wakionyesha mtoto aliyezaliwa na miguu sita kutoka India.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Nilitazama kipindi kizima katika Science Channel juu ya mabinti hawa. Wanasayansi walikuwa wanashangaa wakati mabinti hawa walipokuwa wakijifunza kuendesha gari. Waliweza na walipata leseni yao bila matatizo. Kipindi kilizungumzia maswali mbalimbali likiwemo la ngono na kifo. Mmoja akifariki itakuwaje? Ajabu kweli!

Kilichonifurahisha ni kwamba mabinti wenyewe wana maisha ya furaha tena ya kawaida japo wanahitaji usaidizi mdogo hapa na pale. Halafu nikajilinganisha nao na kugundua kwamba sisi wengine pengine hatuna hata haki ya kupiga makelele na kulalama kwa vitatizo vyetu vidogo vidogo tunavyopambana navyo.