Sunday, 20 June 2010
NI KWELI PESA NI CHANZO CHA MAOVU?
Pesa wewe unaabudiwa kuliko Mungu,unapendwa zaidi ya chochote katika ulimwengu huu,wengine wanakuita Sabuni ya roho,wapo waliowasaliti wenzi wao kwa sababu yako wewe PESA....Leo nimekaa na kujiuliza, hivi ni kweli pesa ni chanzo cha maovu? Tunaona watu wanauana(mfano wanandugu wanapoamua kutoana uhai ili mmoja wao aweze kurithi mali walizoacha wazazi,au mke/mume anapoamua kumuua mwenzie ili aweze kufaidi peke yake mali walizochuma pamoja,kuiba kutokana na ugumu wa maisha au tamaa,kinadada kujiuza,kubaka watoto wadogo kwa sababu mganga kakuambia ukibaka kabinti ka miaka mitano utakuwa tajiri,watu wanauza madawa ya kulevya,wanaajiri watoto wenye umri mdogo kwa sababu hawana gharama,kuchuna ngozi za binadamu wenzao.Na mengine mengi... maovu yote haya yanatendeka mwisho wa siku hawa wote wanachotaka ni PESA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
huo ni ushamba fulani.
Ninaye ndugu akikosa hela anakonda. Yaani hata kama hana we mpe tu akushikie...hatazigusa wala kuzitumia lakini kama alikuwa anaumwa atapona :-(
Ulimbukeni mwingine bwana, acha tu!
Bora mkulima wa kijijini, anayepata mahitaji yake kutoka kwenye shamba, mafuta nk anapata kwa biashara ya kubadilishana mazao!!
Post a Comment