Mpiga picha bora za harusi kwa sasa nchini Tanzania, John akiangalia kwa
makini kazi nzuri za Mwanzo Milinga kwenye maonyesho yaliofanyika leo
tarehe 9/8/2012 pale Alliance Francaise.
Asia Mbwana mwanafunzi wa Mwanzo Milinga akichukua matukio muhimu katika maonyesho hayo
Mwanzo Milinga akiwa na mwanae George wakisimama mbele ya baadhi za kazi
nzuri alizofanya.(Photo Exhibition on Pastoralist Maasai)
Mwanzo Milinga akibadilishana mawazo na Adam H.Mzee wa Kamerayangu.blogspot.com
Wanafunzi wa Mwanzo Milinga walijikuta kwa pamoja wana husika kupiga picha moja.
Watu kutoka mataifa mbali mbali walihudhuria maonyesho hayo ya picha yaliyodhaminiwa na Alliance Francaise.
PICHA NA MAELEZO NIMETUMIWA NA ADAM MZEE.
Friday, 10 August 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
4 comments:
Inapendeza kwa kweli ahsante Edna kwa kutokuwa mchoyo/kwa kutushirikisha matukio kama haya....
MAONESHO YA PICHA YAFANA,....au sio natumai ingekaa vyema'
Unajua hapa wengi tumezoea kusema `maonyesho' lakini angalia neno hilo `kuonyesha'..linatokana na neno `onya'
Ili liwe sawa tunatakiwa tuseme, `kuonesha' ili litokane na neno `onesha' ambacho nafikiri ndicho kiswahili sahihi.
Au sio jirani yangu!
Jirani yangu Emu-Three asante kwa shule ya bure...kiswahili ni chetu lakini kinatupiga chenga mweeeh.
Da Yasinta asante na wewe mdada wangu.
Steve,thanks for dropping by...promise to visit your blog.
Post a Comment