Ni
muda mchache umebaki kabla ya kufikia kilele cha kampeni ya miezi
mitatu (3) ya Nchi Yangu , Wajibu Wangu UTAIFA KWANZA, changamoto ni
nyingi sana tu lakini jambo moja lipo wazi kichwani mwangu, hili
litafanyika, matembezi ya kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro, takribani
200km na zaidi, ikiwa ni uhamasisho na alama ya kuweka mbele maslahi
yaTaifa letu kwanza, kutokuruhusu kutumiwa kwa maslahi ya wengine ama
wachache, kuheshimu na kurudisha misingi ya maadili, heshima na dhamana
ya uongozi na kubwa zaidi kubadilisha mtazamo wetu wa FIKRA, hatuhitaji
kuwezeshwa, kusaidiwa, kudhalilishwa na mwisho wa siku rasilimali adimu
za Taifa letu kuchukuliwa kwa jina la misaada ya wahisani, FUNGUA FIKRA
MTANZANIA, UMASIKINI WETU NI FIKRA ZETU,
Nimebahatika
kutembelea zaidi ya mikoa /kanda kumi (10) nimeonana, kuongea, kukutana
na hata kufanya mahojiano na watoto mpaka waz, vijana hata vikongwe,
watumiaji wa madawa haramu ya kulevya, watumiao miili yao, watoto
waishio katika mazingira magumu, wanafunzi hata wafanyabiashara,
TANZANIA ZAIDI YA UIJUAVYO,
Nimeweza
kufanya mahojiano zaidi ya ishirini na vyombo mbalimbali vya habari
(shukrani kubwa kwao), na nimekuwa nasisitiza ndugu zangu Watanzania,
tuko tayari kuishi kwenye nyumba za vioo angali wenzetu wakiishi juu ya
mawe? AMKA TANZANIA,
Nchi Yangu , Wajibu Wangu UTAIFA KWANZA
Matukio-Amani OleAfrika Aranyande M
Simu : +255 772 54 55 62
Barua Pepe : kwetutanzania@yahoo.com
0 comments:
Post a Comment