Bibi Atupele pembeni akiwa na Mjukuu wake kwenye picha
ya Pamoja...Bibi huyo anaedhaniwa Mchawi
Baada ya vitendo vya kichawi kukithiri kijijini hapo....
Ni Baada ya Mtoto wa Miaka 11 kupotea Ghafla baada tu
ya kuena kumsalimia Bibi huyo Nyumbani kwake Majira ya
Ya Saa 11 Jioni.....!!
Bibi Huyo mwenye Umri wa Miaka (60) aishie kata ya masewe
wilayani Ilemi Mkoani Mbeya...Jana alinusurika kifo Baada
ya wananchi wenye Hasira kali kuchoshwa na Vitendo vya
Kichawi vinavyoendelea kijijini hapo na vyoye Bibi huyo akiusishwa..
Walisema katika vikao kadhaa vilivyoitishwa mtaani hapo kwa
ajili ya kutafuta mbinu za kupatikana kwa mtoto lakini Mwanamke
huyo hakuonesha ushirikiano jambo ambalo lilizua hofu
miongoni mwa wakazi hao hali iliyopelekea kuhisiwa
kuhusika na tukio hilo.
Walisema katika kikao kilichofanyika Machi 23 Mwaka huu
majira ya Asubuhi mtaani hapo wananchi hao waliendelea
kusisitiza kuwa Mwanamke huyo achukuliwe hatua kwa
kuwa ndiye anayehusika na upotevu wa motto ambapo
iliamriwa kwenda nyumbani kwake kufanya upekuzi.
Walisema baada ya kufika nyumbani kwake na kufanya upekuzi
walikuta vitu vinavyohisiwa kuwa vinahusika na ushirikina
ambavyo ni vitovu vya watoto wachanga watatu ambapo
Mwanamke huyo baada ya kuulizwa alishindwa kutolea
ufafanuzi hali iliyosababisha wananchi kupandwa na hasira
na kuanza kumpiga.
Kutokana na tukio hilo Kaimu Mwenyekiti wa Mtaa huo Nedy
Mwamlima alimnusuru Mwanamke huyo katika kipigo
kutoka kwa wananchi kwa kumpeleka katika kituo kikuu
cha Polisi kwa usalama zaidi.
Baada ya mtuhumiwa huyo kunusuriwa na kukimbizwa
katika kituo cha Polisi wananchi hao hawakupoza jazba
zao ambapo waliamua kuteketeza nyumba ya mtuhumiwa
ikiwa ni pamoja na kufyeka mazao yaliyokuwa yamepandwa
jirani na nyumba yake.
Hata hivyo hasira za wananchi hao hazikuishia hapo bali
walimsakama Mwanamke mwingine aliyejulikana kwa jina la
Agnes Sika ambaye ni mke wa Mchungaji wa kanisa la Pentecost
Groly kwa madai kuwa ni rafiki wa mtuhumiwa na amekuwa
akimfichia siri.
Jeshi la Polisi liliwahi kufika eneo laTukio na kumnusuru
Agnes asipatwe na madhara ikiwa ni pamoja na kutochomewa
nyumba yake ambayo tayari wananchi hao walionekana
kuikimbilia kwa ajili ya kutaka kuibomoa.
Aidha Jeshi la polisi linaendelea kumshikilia mtuhumiwa
kwa ajili ya mahojiano zaidi pamoja na upelezi ambapo Baba
mzazi wa Mtoto anayesadikiwa kupotea katika Mazingira ya
kutatanisha akisema anamwachia Mungu baada ya juhudi
za kumtafuta kushindikana.
|
3 comments:
Swali ni je kama sio mchawi kweli itakuwaje, ukizingatia huo uzalilishwaji....Na huu uchawi kwanini usiboreshwe ukawa wa kisayansi, na uwe wa manufaa zaidi. Kwa mfano nasikia watu wanaweza kutembea na ungo, sasa kwanini wasiboreshe huo usafiri, tukawa tunasafiria kwa ungo. Tungewazidi hata wazungu...just imagine...mpo juu na ungo, ....Lkn kitu kikiitwa `uchawi' ..basi tena ni uharibifu tu.
mpaka leo kunawatu wanaimani hizo by www.eliabu.blogspot.com
Jirani Emu-Three hata mimi nimewaza hivyohivyo,ila itakuwa ngumu kwa serikali kuhalalisha kwa sababu wanasema uchawi ni kitu kisichonekana.
@Furaha Eliab-wapo sana hasa hasa vijijini.
Post a Comment