SHIRIKA
la Kijerumani la Friedrich Ebert Stiftung (FES), limekipongeza na
kukisifu Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuendelea kujenga utawala bora
na kujenga amani ya nchi.
Akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara, Philip Mangula,
Mkurugenzi
Mkazi wa FES nchini, Rolf Paasch, alisema shirika lake linatambua
juhudi na kazi inayofanywa na CCM katika ujenzi wa demokrasia na amni ya
Tanzania.
Paasch alisema Tanzania ni nchi muhimu katika
historia ya bara la Afrika hususan mchango wake katika ukombozi wa nchi
zilizo kusini mwa Afrika, hivyo inapaswa kuwa mfano na kuhifadhi
kumbukumbu muhimu za kihistoria kuhusu ukombozi.
"Ni mara
yangu ya kwanza kuja Tanzania na nafurahi leo kukutana nawe kiongozi wa
juu wa CCM, kwa niaba ya FES naahidi kuimarisha na kuedndeleza
ushirikiano uliopo baina yetu na CCM na Tanzania kwa jumla," alisema.
Kwa
Upande wake Mangula, alisema katika kuhakikisha Tanzania inatunza
kumbukumbu muhimu za kihistoria za bara la Afrika, kwa makubaliano na
nchi zingine za bara hilo zimeamua kutenga eneo maalumu wilayani
Bagamoyo kwa ajili ya ujenzi wa kijiji cha kumbukumbu hiyo.
Mangula
alimwambia mkurungenzi mkazi huyo kuwa tayari eneo hilo limeshapatikana
na kwamba mchakato wa hatua zaidi katika kuelekea ujenzi wake kwa
kushirikiana na nchi nyingine, unaendelea
HABARI NA PICHA NIMEUMIWA NA ADAM MZEE.
1 comments:
Hoja ya kumbukumbu ni nzito sana, nahisi tusipoangalia tutajikuta watoto wetu hawakumbuki ni nini kilitokea kwenye vita vya majimaji, maana hata kwenye redio, au tv, tarehe kama ya leo...husikii wakitaja mambo ya kikwetu.
Post a Comment