MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam imemhukumu mfanyabiashara Bw. Mohamed Yusuph (27), mkazi wa Kariakoo kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka 11.
Kabla ya hukumu hiyo kutolewa, mahakama iliamuru mshitakiwa huyo kufungwa kifungo cha maisha kutokana na uzito wa kosa lakini baada ya mshitakiwa kuomba apunguziwe adhabu kutokana na matatizo ya kiafya iliamuru aende jela miaka 30.
Mwendesha Mashitaka Mkaguzi wa Polisi, Bw. Musa Gumbo alimtaka Hakimu kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo.
Akitoa hukumu hiyo Hakimu wa mahakama hiyo Bi. Janeth Kinyage alisema ametoa hukumu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka ambao unamtia hatiani mshitakiwa.
Awali ilidaiwa kuwa Februari 21 mwaka jana, maeneo ya Feri mshitakiwa alimalawiti mtoto wa miaka 11 na kumsababishia maumivu makali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comments:
hiyo 30 haimtoshi,tamaa gani ukabake mtoto wa miaka 11?
Post a Comment