Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday 18 March 2010

KUKOROMA HUSABABISHWA NA NINI?

Hivi kukoroma husababishwa na nini? na nini dawa yake? na je yeye huwa hajitambui kuwa anakoroma? do you know how it feels to live with someone who is snoring? Oooh good Lord......Jamani mimi napata tabu sana na huyu jirani yangu yaani akianza kukoroma hadi aliye chumba cha pili atasikia jinsi anavyokoroma kwa nguvu.Can somebody help me plizzzzzzz kama kuna dawa ya kuzuia.

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Edna! nimewahi kusikia kuna dawa kwenye duka la madawa nenda tu kaulizia ila samahani jina nimelisahau. Pole sana maana hii inakorofisha sana usingizi.

EDNA said...

asante da Yasinta nitaenda uliza.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Edna, sina hakika kama kuna dawa labda ughaibuni. Lakini ninachojua ni kuwa huwa kuna misuli fulani imelegea na hivo inabidi ikazaawe kwa mazoezi ambayo hayahitaji dawa za dukani.

Hebu soma hapa na mjaribu kabla ya kununua dawa.

Okey!

Christian Bwaya said...

Nilishawahi kukaa chumba kimoja chuo na bwana mmoja mkoromaji. Aisee!

Ulikuwa ni mwaka mwaka mmoja wa mateso. Lakini baade tulikuja kubaini kwamba dawa nzuri na ya kuaminika ni kuchukuliana naye.

Sasa sijui kama hiyo yaweza kutafsirika kama dawa kwako dada Edna? Mkubali, halafu utashangaa kukoroma huko kutakuwa burudani fulani ya kukuchekesha na sio kukera.

Simon Kitururu said...

Kukoroma husababishwa na mambo mengi kwa hiyo kama hujui kukoroma kwake kunasababishwa na nini sikushauri uende tu duka la dawa kununua dawa.

Kumbuka wengine sababu ya kukoroma ni kwamba ni matipwatipwa aka wanene. Kwa hiyo kama kukoroma kwako ni kule kusababishwako na UNENE hata ununuliwe dawa gani kama hupunguzi unene kukoroma kutakuwa palepaele.

Na kukoroma kwingine dawa yake ni kukwepa kulala chali au kifudifufi na kulalia upande ili kuepusha ulimi kuziba koo. Lakini kumbuka mara nyingi akoromaye hajisikii kwa hiyo ni vigumu kumfanya alale kinamna fulani hasa kama sio yule mpenzi msheaye naye kitanda.

Na kumbuka kukoroma kunaweza kuwa ni dalili tu ya kuwa mtu anaugonjwa fulani ambao huo ndio uhitajio tiba kwa hiyo ushauri wangu mtu amwone dakitari na sio tu kukimbilia dawa kwa kuwa unaweza kukuta unakimbilia kutibu dalili na kuacha ugonjwa.