Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Sunday, 25 July 2010

Aomba apunguziwe mpaka bure......Cheka unenepe.


Jamaa mmoja toka bushi aliingia mjini na kufikia kwa ndugu yake, katika tembea tembea yake alimtembeza sehemu zote muhimu kama Kariakoo mtaa wa Kongo na Soko la Karume.
Baada ya kulifahamu jiji kidogo, siku moja alimuomba ndugu yake pesa aende akanunue vitu. Ndugu yake baada ya kumpa pesa, alimueleza;

“Unajua mjini wanauza nguo kulingana na muonekano wako, sasa mtu akikuuzia nguo usikubali moja kwa moja, komaa naye akupunguzie lazima utanunua kwa bei ndogo.”
Baada ya maelekezo jamaa aliingia mitaa ya Mchikichini na kukutana na jamaa anauza viatu.

“Viatu bei gani?”
“Elfu 22.”
“Aah, nipunguzie bwana.”
“Leta basi ishirini.”
“Nipunguzie bwana.”
“Wewe mnunuzi kweli?”
”Ndiyo.”

“Basi leta 15.”
“Nipunguzie bwana.”
“Bei ya mwisho 10.”
“Nipunguzie bwana.”
“Kila bei nikupunguzie, basi chukua bure.”

“Aah, nipunguzie bwana.”
Muuza mitumba aliamini yule jamaa hakuwa mzima anapoomba apunguziwe hata bure.

4 comments:

Born 2 Suffer said...

Si kucheka hapa ni mpaka lini Africa tutavaa mitumba nasikitika sana yani.

Yasinta Ngonyani said...

Edna! nimecheka na nadhani likizo yangu imeanza na baraka. Ahsante,Kaazi kwelikweli:-)

chib said...

Yaani, sijui huyo nimuite zezeta au, ha ha haaa

emu-three said...

We wafikiri angempa bure kama sio utani wa wauaza mitumba. Lakini katika maisha halisi ndivyo tunavyopenda vya bure, na kushindwa kujua kuwa vya bure navyo vina gharama.
Jamaa mmoja alienda kwa muchuza samaki katika kuhangaika kupungiziwa akajikuta anapewa bure, kumbe mwenzake alishaona samaki wale ni wabaya, wameshaharibika, na maeneo yao sehemu ya kutupa taka haipo, sasa akaona huyu ndiye atakuwa shimo la taka, akampa bure.
Jamaa kufika ndani ya daladala harufu ikawa haitamaniki, kila mtu akaziba pua mapaka ikawa nyekundu, mwishowe watu wakashindwa kuvumilia na kumuomba konda amshuse yule jamaa.
Alishuka kabla hajafika, kahangaika kutafuta usafiri, lakini kila gari alipolikaribia likawa linaondoka hata bila kumuuliza wapi unapokwenda. Ikabidi achukue bodaboda, akalipia gharama kubwa zaidi ya zile samaki..
Kafika nyumbani, mkewe aksema mimi hawa siwawezi kuwatengeneza inahitajika vikorombwezo kibao, ikabidi imtoke hela, kununua sijui ndimu nk, mwisho wa siku alijikuta kawanunua wale samaki kwa bei mara mbili ya bei yake...