Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday, 22 July 2010

HII NDIO BONGO DAR ES SALAAM.


Bongo Dar es salaam ni tambarare popote pale ni jalala,Angalia lundo la takataka lilivyotulia pembeni ya barabara....Lawama tumtupie nani? jiji (serikali) kwa kuwa hawajaweka sehemu maalumu za kutupa takataka? au hao watu wanaotupa takataka hapo kwa makusudi?.Au ndio tunasubiri mpaka kipindupindu kitupindue ndio tutaanza kuchimba mashimo.

3 comments:

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

lawama tunakutupia wewe mwananchi ambaye unatupa taka hapo!

Pia wewe ambaye unalipa kodi bila kujua inakwenda wapi na itatumikaje.

Pia wewe ambaye unachagua viongozi kwa bakshishi ya fulana, kofia, kanga na chumvi :-(

Yasinta Ngonyani said...

Bado sana, kwa kweli magonjwa mengine tunayakaribisha wenyewe. Hapo sasa si kuilaumu serikali , kweli hata kuweka pipa tu tunashindwa... sisemi sana kwani inaumiza..

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Naunga mkono hoja ya Ng'wanambiti. Hata hivyo napata kigugumizi kumlaumu mwananchi anayetupa taka hapo. Kama hakuna mahali pa kutupia taka, tunategemea hizo taka akazitupe wapi? Nilitembea Arusha na ganda la chungwa kwa muda mrefu sana mfukoni kwa sababu hapakuwa na mahali ambapo ningeweza kulitupa bila kuchafua mazingira. Tazama hapa:

http://matondo.blogspot.com/2010/07/vituko-vya-mtaa-wa-makoroboi-jijini.html