Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Monday 30 August 2010

PALE USHOGA UNAPO KUWA SI USHOGA TENA….!!!!


Amekuwa rafiki yako kwa mda mrefu na mmeshuka na kupanda milima wote mkiwa na mshikamano. Lakini katika maisha yenu yote hamjawahi kuwa na mikwaruzano.

Sasa mmejikuta urafiki wenu upo hatarini kusambaratika chanzo kikubwa ni kutoelewana katiyenu juu ya maswala fulani. Pale hasira zinapo teka akili zenu hali yakupatana inazidi kupotea na dalili za urafiki wenu au ushoga ndio unazidi kuwa katika hati hati ya kufutika.

Chunga sana kabla hamjaamua kufutiana namba za simu, na kusonyana wakati mnapishana mitaani kaeni chini na mjaribu kuyafikiria haya na kuyafanyia kazi yafuatayo.

Tafakarini chanzo cha ugomvi wenu: Tafuta mahali ambapo pametulia nauanze kutafakari nini kilichofanya nyie mfikie hapo mlipo sasa. Jaribu kujikumbusha majadiliano mlio yafanya mpaka yaka sababisha ugomvi wenu. Angalia kama mlicho kizungumza sikiu hiyo ndio chanzo au kuna vitu vingine vimejificha?

Tengenezeni Mipango: tambueni nini mtakacho kizungumza kabla hamjakutana tena. Msikubali maongezi yenu yakawaingiza kwenye ugomvi kwa mara ya pili. Cha muhimu zingatieni maneno ya busara yatakayo wafikisha katika suluisho.

Jitayarishe Kuomba msamaha: Kama utagundua ulifanya makosa basi kuwa tayari kuomba msamaha. Katika urafiki kuwatayari kukubali kosa, kwasababu mwanadamu anatabia ya kukimbia makosa.

Jaribuni kuzungumza point tu: Wakati wa kudiskasi ukiwa umewadia jitahidini kuanza na pointi zihusianazo na utatuzi wa ugomvi wenu.Bila kusahau mambo mlio yafanya pamoja wakati mkiwa katika urafiki mzuri hiyo itasaidia kurudisha kumbukumbu nzuri za urafiki...source Mohamed Dewji blog.

0 comments: