Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday 19 August 2010

Vuvuzela yaingia kwenye kamusi ya Kiingereza

Mashindano ya Kombe la Dunia na hali ya kuyumba kwa uchumi ni mambo yaliyosababisha kujumuishwa kwa maneno mapya katika kamusi ya Kiingereza ya Oxford (Oxford Dictionary of English).

Vuvuzela, ni neno jipya, likiwa na maana ya chombo cha kupulizwa kilichotumiwa na mashabiki wa soka wakati wa mashindano ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.

Vile vile matatizo ya uchumi duniani yameongeza "toxic debt" - deni lenye uwezekano wa kutolipwa.

Kamusi hiyo - tofauti na nyingine ijulikanayo kama Oxford English Dictionary (OED) ilichapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1998 - ina maneno mapya zaidi ya 2,000.

Inakusudia kuainisha mambo ya kisasa katika matumizi ya lugha ya kiingereza.

Toleo lake la tatu lilihusisha maswala ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

2 comments:

John Mwaipopo said...

wajuzi wa lexicography walishajua uingizwaji wa neno vuvuzela katika lugha ya kiingereza. na litaingia katika lugha nyingi tu, kikiwemo kiswahili.

hii ni kwa sababu chombo chenyewe ni kipya, i.e., kimetambulishwa kwa mara ya kwanza katika ulimwengu wa soka. majina yanayokuja na vitu vipya ama uvumbuzi mpya hiungia haraka katika leksikolojia ya lugha husika. mfano wa maneno yanayokuja na uvumbuzi mpya ni video, tv n.k.