Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Monday 23 August 2010

WANAWAKE NA VIATU!

Inasemekana wanawake/wasichana wanapenda viatu kuliko wanaume/vijana na wanatumia pesa nyingi kwenye viatu, I mean mapenzi ya viatu sio mapenzi ya mwanamke na mwanaume).Utakuta mwanamke/msichana mmoja ana pair za viatu zaidi ya hamsini (50) na bado akipita dukani akaona kiatu kizuri atanunua kama hana hela yupo radhi akope,wakati mwanaume anaweza kuwa na pair mbili au tatu tuu za viatu na akaridhika kabisaa.I have to admit i also love shoes so so much... lakini sijafikisha hizo pair hamsini mweeeeeeee.

CHEKA UNENEPE.

Msukuma mmoja alibahatika kwenda zake Uingereza, baada ya kufika alishangaa uzuri wa mji na majengo ya kushangaza.

Ili akirudi Tanzania awakonge wenzake kila alichokiona alitaka kujua kinamilikiwa na nani. Cha kwanza kuuliza kilikuwa kujua uwanja ule wa ndege unamilikiwa na nani. Alimuona Mzungu mmoja amesimama alimfuata na kumuuliza.

“Eti uwanja huu wa ndege ni wa nani?”
“Speak English,” Mzungu hakumuelewa na kumuomba azungumze Kiingereza.

Jamaa baada ya kuelezwa vile aliondoka akiamini anayemiliki ule uwanja ni speak English. Alipoondoka pale alikwenda hoteli moja kubwa na kuulizia ile ni ya nani, aliyemuuliza kwa Kiswahili hakumuelewa alimjibu.
“Speak English.”

Kila kona alielezwa vile, basi jamaa aliporudi Tanzani aliamini Speak English ndiye tajiri mkubwa nchini Uingereza. Kila kona aliwaeleza jinsi kila kona alipouliza watu kuhusu mmiliki wa vitu vya thamani aliambiwa Speak English.

Watu walimcheka na kumueleza Speak English siyo tariji bali walimueleza azungumze Kiingereza kwa vile walikuwa hawamuelewi akizungumza kiswahili.
Mmh, hii kali kujua lugha nako raha.

9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

ha ha ha ahaaaaaaaa ha ha ha ha ahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa nashindwa kuacha kucheka. Kweli kujua lugha ni mali.

emu-three said...

Hahahahaha....., na yeye angekuwa akiwaambia `ongea kiswahili ili na wao wahisi kuwa `ongea kiswahili ' ni zinga la tajiri Tanzania

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

wewe, viatu vyote hivyo vyako?

Anyway, naona unawatafuta wasukuma...miye simo ngoja nijiweke pembeni kwanza....lol!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ni kweli huyu anatutafuta Wasukuma. Ngoja nikatafute utani juu ya Wanyalukolo nije nimshushie dhoruba! Nimecheka sana. Wasukuma huwa tunataniwa sana kuhusu ushamba, kutoenda shule na mengineyo. Ni kweli kuchunga ng'ombe kulitupumbaza lakini lakini sasa kumekucha na mambo yanabadilika kwa kasi (ingawa mkoa wa Shinyanga bado ni wa mwisho katika elimu!). Muda si mrefu hatutaamini tena kwamba Speak English ndiye tajiri mkubwa...

KUHUSU VIATU...

Imelda Marcos - Mke wa Ferdinand Marcos aliyekuwa dikteta wa Phillipines alikuwa na zaidi ya pea 2,500 za viatu. Wengine mtafikia hapo?

mumyhery said...

Du umeshinda mwanawane tuma salam!!!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Bwana Matondo naomba ubadilishe neno UEMPTY kwenye bendera ya Mizengwe na kuweka AN EMPTY. Kidogo umeteleza.
Kila la heri ila nami namjua huyo jamaa aitwaye Speak English anaishi kwenye mji mmoja uliojaa watu wanaojisifu na kusifika kwa kuwatawala, kuwafitini na kuwaibia wenzao. Uwanja wa ndege wa Heathrow unamilikiwa na jamaa mmoja msukuma aitwaye Andrew Chenge toka Unyantuzu. Upo hapo mwanawane?

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Bwana Matondo,
Naomba ubadilishe neno UNEMPTY kwenye bendera ya Mizengwe na kuweka AN EMPTY. Kwani umeteleza kidogo. Kuhusu utani wa wasukuma ni kweli namjua huyo Bwana aitwaye Speak English. Anaishi kwenye nchi ya wazushi na wafitini wanaosifika kwa kuwatawala na kuwaibia wenzao. Ule uwanja na hoteli vinamilikiwa na msukuma mmoja toka unyantuzu aitaweye mzee wa vijisenti aka Andrew Chenge na mhindi wake aitwaye Vinyeshi Virani Seileshi.