Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday, 26 August 2010

YUPO KAZINI!


Watu wamemuamini MUGAMBO na kumkabidhi mali zao na usalama wao ,lakini jamaa kauchapa usingizi kama hayupo kazini vile..... Mwizi akija atajichukulia kila kilichopo kiulaiiini.Alafu silaha aliyokuwa nayo ni kirungu, sasa imagine limekuja jambazi na bastora sijui itakuwaje mmmmh.

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

basi utakuwa mwisho wake wa kuishi duniani hapa. Kazi kwelikweli.

SIMON KITURURU said...

Maisha ni magumu sana Bongo. Nawajua mgambo kama hawa wawili. Na tokea asubuhi wanajishughulisha na mambo ya shamba ili msosi ueleweke halafu usiku inabidi wakalinde ili pia angalau watoto waende shule.:-( Wengi sio nia yao kulala ila unaweza kukuta hapo ndio chansi pekee ya kulala kabla ya kurudi tena kuhangaika na maisha.

Na mmoja kati ya wawili niliosema nawajua , MKE wake kidogo tu hakawii kumlalamikia kuwa ni mvivu ndio maana hana pesa kama wenzake ingawa ukichukulia kuwa siku ina saa ishirini na nne tu hata sijui afanye nini zaidi ya kuiba ili kieleweke.:-(
Kuna wezi pia waibao kwa kuwa inabidi tu waibe.:-(

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

mlinzi pekee wa mali yako ni wewe mwenyewe, au vipi?

Uwe na wakati mwema sana dadito!

John Mwaipopo said...

walinzi wengi ni wadokozi/wezi sehemu wanazolinda