Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Monday 20 September 2010

JE NI KWELI NCHI ZA AFRIKA ZIMEFANIKIWA KUPUNGUZA UMASIKINI?



Umoja wa Mataifa umesema kuwa nchi za Afrika zimepata mafanikio kadhaa katika kupunguza umaskini kwa kipindi cha miaka kumi, tangu viongozi wa dunia walipoweka malengo ya milenia ya maendeleo.

Akizungumza mjini New York kabla ya kikao cha kutathmnini mafanikio yaliyofikiwa tangu mwaka 2000, naibu mkurugenzi wa Umoja wa Mataifa wa uhamasishaji wa malengo hayo barani Afrika Charles Aburge amesema ukuaji wa uchumi barani Afrika umesababisha kufikiwa kwa malengo hayo katika nchi nyingi.

Lakini Afrika inaendelea kuathiriwa chini ya kile kinachoitwa uchumi huria ambao haudhibitiwi na kodi zinazotozwa na nchi tajiri.

1 comments:

Simon Kitururu said...

Inachekesha ukikuta MATAJIRI wanajadili nakufikia HITIMISHO kuhusu umasikini wasiouishi au labda hata kuujua.:-(