Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday 14 September 2010

KUMBE POMBE PIA NI CHANZO CHA WATOTO WA MITAANI?

Hilo sio shimo bali ni makazi ya watoto wa mitaani yaani hapo ndipo mahali wanapolala....



Wakizungumza na mwandishi wa habari walisema sababu zilizowafanya watoke majumbani mwao ni kutokana na ulevi wa wazazi wao hasa kina baba. ”MIMI NIMETOKA NYUMBANI KWA SABABU BABA YANGU NI MLEVI NA ANAMPIGA MAMA KILA SIKU HADI MAMA AMEENDA KWAO NA MIMI NAPIGWA KILA SIKU BABA YANGU MIMI NI MLEVI HASWA” MMOJA WAO ALISEMA.
Source Mohamed dewji.

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Tumesema mara nyingi kuwa pombe si maji. Kama mtu unaona huwezi kujiheshimu unywapo pombe kwa nini usiache tu. Maana sasa inaonekana kama unamnywea mtu fulani. Kunywa kwa ustaarabu sio kwa ajili ya kumpiga mtu. Pole sana watoto kuwa na makazi kama hayo inasikitisha sana kwa kweli.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

napenda pombe jamani mbona mnakuwa hivyo? ...lol!

Simon Kitururu said...

Pombe pia ni chanzo cha watoto mitaani kwa kuwa pia wako wajistukiao wameshapata mimba AU KUMPA mtu mimba mitaani bila hata kujua au kuwa na kumbukumbu ya waliyoyafanya ya KIKUBWA wakati wamelewa huko mtaani.:-(

emu-three said...

Pombe ni chachizo la maasi kichwani, mlevi hana aibu na anaweza akafanya machafu ambayo hangeweza kuyafanya akiwa mzima.
Ni kweli watoto wengi wanakimbia fujo za wazazi wao ambao wamebobea katika ulevi. Fikiria hiki kizazi kitaenda wapi na nini matokeao yake ya baadaye...